Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Ernest Semayoga: Kutoka muuza unga mpaka mhitimu wa digirii gerezani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Image
WASWAHILI walisema elimu haina mwisho lakini sasa imethibitika licha ya kutokuwa na mwisho, elimu haichagui mahali, nafasi wala mazingira kama inavyodhihirishwa mfungwa wa miaka kumi gerezani, Ernest Semayoga ambaye licha ya kuishi chini ya uangalizi na sheria za magereza zinazozuia uhuru wake, amefanikiwa kupata Shahada ya Sheria yenye heshima. Ndivyo ilivyokuwa Desemba mosi mwaka huu ambapo Ernest aliweka historia katika familia yao ya marehemu Michael Tiliniga Semayoge na Tibus Tiliniga waliokuwa maarufu kama mama na baba Nzingo wakati walipokuwa wakiishi eneo la Mwanga mkoani Kigoma. Mungu awalaze pema peponi wazazi hao wa watoto saba ambao kama wangekuwepo siku hiyo, wangerudisha faraja mioyoni mwao waliyokuwa wameipoteza hasa baada ya kusikia mtoto wao wa sita, Ernest Semayoga kahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela nchini Malaysia. Kama wangekuwepo hai siku hiyo, tumaini kwa mtoto wao lingerudi upya baada ya mtoto wao huyo kutunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) huku akiwa amebakiza takribani miezi tisa tu kutoka gerezani baada ya kukamatwa nje ya nchi akifanya biashara ya dawa za kulevya. Ni historia kwa familia zaidi kuliko taifa kwa kuwa yeye si wa kwanza kupata shahada akiwa gerezani kwani mwaka juzi mfungwa mwingine Haruna Gombela, ambaye anatumikia adhabu yake ambayo itaisha mwaka 2025, ndiye aliyekuwa wa kwanza kupata shahada akiwa gerezani na sasa anajipanga kuchukua Shahada ya Uzamili ya Sheria (LLM) kutoka OUT. Semayoga (37) ambaye ni kijana mtanashati aliyezaliwa mwaka 1972, alitunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk. John Malecela katika hafla ya pekee iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Tolly Mbwete, Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha, Mkuu wa Magereza, Kamishna Augustino Nanyaro na wafanyakazi mbalimbali wa OUT na Magereza. Sherehe hiyo iliyopambwa na bendi ya Polisi pia ilihudhuriwa na ndugu wa Semayoga, waandishi wa habari pamoja na wanajeshi waliokuwa wakitumbuiza katika hafla hiyo kwa bendi yao. Semayoga, ni mmoja wa wahitimu wa mwaka huu wa Chuo Kikuu Huria (OUT) katika sehemu ya pili ya Mahafali ya 21 ya chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Kikosi Maalumu cha Kuzuia Ghasia Magerezani, Ukonga, Ilala, jijini Dar es Salaam. Mahafali hayo yalifanyika katika nyakati mbili tofauti ambapo mfungwa huyo alifanyiwa ya kwake Desemba mosi tofauti na wahitimu wenzake waliofanyiwa ya kwao Novemba mwaka huu kutokana na masharti ya Sheria za Magereza. Kijana huyo mwenye mke na mtoto mmoja anayeitwa Astrida Michael anayesoma kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya St. Mary iliyoko Mbezi jijini Dar es Salaam alipopata wasaa wa kuzungumza, baada ya kupata shahada yake kwa kujiamini aliiomba serikali iwasamehe wafungwa waliojirekebisha.
Tags:

0 comments

Post a Comment