Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - CCM yanawa mikono kwa mashambulizi ya Sophia Simba

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
CCM yanawa mikono kwa mashambulizi ya Sophia Simba
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, chama chake hakihusiki na mgogoro unaomhusu kada wake Sophia Simba.
*Hakihusiki na mgogoro wake na Anne Kilango

Na Joyce Mmasi

CCM imeamua kutoingilia mgogoro baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Sofia Simba na Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango, kwa maelezo kuwa unawahusu wao wenyewe na kwamba; hakuna miongoni mwao aliyelalamika kupitia taratibu za chama.

Msimamo huo umetolewa siku chache baada ya ugomvi mkubwa kuibuka katia ya kada hao wa CCM, baada ya Simba kumtuhumu Anna Kilango mambo mbalimbali katika kikao cha Kamati ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kilichofanyika mjini hivi karibuni.

Simba alidai ndani ya kikao hicho kwa harusi ya John Malecela na Kilango ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.

Simba anadaiwa kusema katika kikao hicho cha kuwa Kilango siyo msafi na kwamba kelele anazopiga kuhusu ufisadi zinatokana na kukosa kuwa mke wa rais.

Hata hivyo, Kilango hivi karibuni alisema amedhamiria kufikisha mahakamani Waziri Simba kwa madai ya kudhalilishwa.

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliambia Mwananchi Jumapili wiki hii kuwa ugomvi wa wanawake hao, ambao pia ni wanachama wa Jumuia ya Wanawake (UWT), haukihusu chama hicho.

Makamba alisema hayo baada ya kulizwa msimamo wa CCM baada Kilango kutishia kwenda mahakamani kumshtaki Mwenyekiti wa Simba kwa tuhuma za kumkashifu.

Makamba alisema yuko tayari kuzungumzia jambo lolote linalohusu chama kwa ujumla, lakini si ugomvi wa wanawake hao kwa sababu hataa yeye hajui wanachogombea.

“Umesikia mama, niulize mambo yanayonihusu mimi na CCM; sitaki kuzungumza mambo ya watu…. Ule ni ugomvi wa Sofia na Mama Kilango. Yale ni mambo ya watu sio ya Chama. Elewa hivyo kuwa siwezi kuzungumzia mambo ya watu kwa kuwa hayana faida kwa chama chetu,” alisema Makamba.

Simba ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Taifa, hivi karibuni aliripotiwa kuingia kwenye mzozo na Katibu wake, Husna Mwilima akimtuhumiwa kuendesha kampeni za kutaka kumng'oa katika wadhifa wake.

Hata hivyo, Simba ameripotiwa akisema kwamba mzozo ulipo katika jumuia hiyo unatokana na watu kutaka kuzuia hoja ya kuwa na ukomo katika ubunge wa viti maalum na uongozi wa jumuia hiyo.

Alisema kwamba, hatalegeza uzi katika kusimamia jambo hili ili kuondoa usultani katika ubunge wa viti maalum kuwa wapo waliofanya uwakilishi huo wa wananchi kuwa ni wa kudumu.

Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati alisema suala la ugomvi baina ya wanachama hao halijawasilishwa ndani ya chama, hivyo hawezi kuuzungumzia kwakuwa hana ushahidi juu ya jambo hilo.

“Hilo jambo halijaletwa rasmi kwenye chama, hivyo hatujui endapo ni maneno ya magazeti au yana ukweli kiasi gani. Wacha tuyasubiri kama yapo wakiyaleta kwenye chama ndipo tutakuwa na lakusema," alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Alisema pamoja na kwamba Kilango na Simba ni wanachama wake, lakini hawawezi kuzungumzia au kutolea maelezo mambo yanayowahusu bila kufikishwa ofisini kwake.

Alielezea suala la ugomvi huo kuwa ni sawa na maneno yanayovumishwa tu barabarani ambayo wakati mwingine ukiyachunguza utabaini kuwa hayana ukweli.

Wakati viongozi hao wa chama wakinawa mikono kuhusu ugomvi wa makada wao wa CCM, hali ndani ya chama hicho haijatulia kutokana na mgawanyiko mkubwa kuzidi kuongezeka.

Tags:

0 comments

Post a Comment