Vyombo vya habari duniani vyagawanyika kuhusu ushindi wa Rais Obama
WASHINGTON
Vyombo vya habari duniani vimegawanyika kufuatia mshangao walioupata baada ya Rais Barack Obama wa Marekani kutangazwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, kwa mwaka huu wa 2009. Baadhi ya vyombo vya habari vimepongeza ushindi huo vikisema Rais Obama amekuwa mfano bora, huku vingine vikikosoa ushindi huo unaonekana kuwa wa kisiasa.
Jana, kamati ya Nobel mjini Oslo, ilimtangaza Rais Obama mshindi wa tuzo hiyo kutokana na juhudi za kipekee za kiongozi huyo wa Marekani katika kuimarisha diplomasia ya kimataifa na kupigania ulimwengu usiokuwa na silaha za nyuklia. Hata hivyo, viongozi mbalimbali duniani wameendelea kutoa pongezi zao kwa Rais Obama kufuatia ushindi huo. Hata hivyo Rais Obama ameamua kutoa zawadi ya fedha zinazoambatana na tuzo hiyo ambazo ni dola milioni 1.4 kwa mashirika ya misaada.
0 comments