Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mshitakiwa aibua mabishano ya kisheria mahakamani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

MAELEZO ya mshitakiwa wa sita katika kesi ya kupora Sh 234 mali ya benki ya NMB, Tawi la Moshi aliyoyaandika polisi na kukiri kushiriki katika tukio hilo, yameibua mabishano makali ya kisheria mahakamani baada ya mawakili wa utetezi kupinga vikali maelezo hayo, yasipokelewe kama kielelezo.

Mabishano hayo, yaliibuka jana mchana baada ya shahidi wa nne upande wa mashitaka, Mrakibu Msaidizi wa Polisi(ASP), Isaya Mbugi kutoa maelezo hayo, kama kielelezo mbele ya Jopo la Mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Hakimu Mkuu Mkazi, Pantrine Kente.

Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Moshi,Juma Ramadhan, Shahidi huyo alisema aliandika maelezo hayo ya kukiri kosa la mshitakiwa wa sita, Emanuel Mziray na kwamba aliyatoa kwa hiyari yake na alimweleza haki zake zote, ikiwamo kumuita wakili wake au ndugu yake yoyote kushuhudia.

Shahidi huyo ambaye ni mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Same (OCS), alisema pamoja na kumfahamisha haki zake hizo, mshitakiwa huyo alimweleza kuwa kulikuwa hakuna haja ya kuwepo mtu mwingine na ndipo alipochukua maelezo hayo.

Haya hivyo, Wakili Midian Mwale anayemtetea mshitakiwa huyo pamoja na washitakiwa wengine, alipinga vikali maelezo hayo kwa kuwa mteja wake, ameikana saini iliyoko katika maelezo hayo, akidai polisi wameigushi.

Pia wakili huyo, alisema kifungu cha 57 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai (CPA) kina maelezo kama hayo kwamba yanaweza kupokelewa mahakamani endapo tu mshitakiwa huyo angekuwa ana ushahidi ambao unatofautiana na maelezo yake aliyoyatoa wakati akihojiwa na afisa wa polisi.

Mwale alidai sheria hiyo, inasisitiza kuwa maelezo ya ungamo la kukiri kosa yanapaswa yaandikwe katika mfumo wa maswali na majibu tofauti na maelezo hayo yanayotakiwa kutolewa mahakamani kama kielelezo.

Wakili huyo alisema kisheria, upande wa mashitaka ulipaswa kutoa notisi ya kutoa maelezo hayo kama kielelezo na washitakiwa wote wapewe nakala ya maelezo hayo ili kama maelezo hayo yanawagusa basi wapate fursa na haki ya kisheria ya kuwasilisha pingamizi la kupinga kupokelewa kwa maelezo hayo.

Akijibu hoja hizo, Wakili Ramadhan alisema wakili mwenzake, Mwale anapaswa kusoma vifungu vya sheria kikamilifu badala ya kushikilia kifungu kimoja cha 57, wakati kifungu cha 58 cha sheria hiyo, kinatoa maelezo jinsi ya kuchukua maelezo kama yalivyochukuliwa na ASP Isaya.

Wakili huyo wa Serikali alisema maelezo ya mshitakiwa kukiri kosa yanaweza tu kupingwa yasipokelewe kama kielelezo endapo tu mshitakiwa atakuwa ameyatoa bila hiyari yake au kwa kushawishiwa.

Tags:

0 comments

Post a Comment