Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - MSAADA KWENYE TUTA..................

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter UFAF ANUZI WA HOJA YANGU NILIYOITOA KATIKA MKUTANO MKUU TSU(10/9/O8).

DIPROMASIA ITUMIKE KAMA CHOMBO CHA KUTATUA MATATIZO

Ndugu wanafunzi wote wa Tanzania –chuo Lumumba (Russia)

Napenda kuwasalimia , na poleni kwa majukumu kwa kila mmoja kwa nafasi yake!

Kwanza , napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kuupongeza uongozi wa TSU-Lumumba chini ya Bwana kanyathare Boniphace kwa kazi nzuri wanayoendelea nayo ya kurejesha umoja wa watanzania hapa chuoni, bila kujali mawazo ya wachache yasiyo na dira wala muelekeo.

Uongozi wa TSU, ni halali, na ulichaguliwa kwa misingi ya kidemokrasia(uchaguzi mkuu) na utakuwa madarakani na kufanya kazi yake kwa kufuata misingi ya katiba . Mimi kama Mtanzania na mwanachama wa TSU ,SINA BUDI kuheshim na kulinda umoja wetu tukiongoza na viongozi wetu halali.

Napenda kutamka wazi kuwa sina chuki na uongozi wa TSU na sitakuwa na hata chembe ya hisia hizo kama wengi wenu mnavyodhani, nina uheshimu uongozi na ninawaheshimu watanzania wote kama ndugu zangu, lakini tuzingatie kuwa kukubali kukosolewa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. “No one is perfect exactly”

Pili , napenda kutoa ufafanuzi wa hoja niliotoa katika mkutano mkuu, -ni kweli nilionge na kunukuliwa baadhi ya sentensi nilipokuwa nachangia mada, nilisema “jumuia yeyote haikosi wendawazim, na TSU kama jumuia kuna wendawazimu ambayo kazi yao ni kuvuruga Amani”…….. nikanukuliwa nikisema- mnajua , kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo………..”njia ya dipromasia itumike zaidi badala ya mgomo unaonekana kushinikizwa na baadhi ya watu.”

Sentensi hizo zinaonekana kuwagusa watu wengi, na wengine kuanza kutoa matamshi ya kashfa kwangu, napenda kusema kuwa :-Sijamkashifu mtu yeyote, na wala sio matusi kusema kama kwenye jumuia kuna wendawazim. Kumbukeni hii ni moja ya Fasihi inayoikosoa jamii ili ijatambue.

Ndugu zangu, napenda tuelewane kuwa hoja iliyoletwa na viongozi wa TSU, ni kuhusu fedha zetu toka serikalini, ambapo mpaka sasa hatujapata ila sasa mapendekezo yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya wajumbe wakiwemo viongozi wa juu wa TSU ni Kufanyika kwa MGOMO, eti ndo njia mbadala ya haraka zaidi kutatua tatizo. Baadhi ya viongozi walinukuliwa wakisema “dipromasia imewashinda katika hili, njia sahihi ni mgomo tu”

Ndugu zangu , tutakuwa si wasomi sahihi, kama mawazo ya mtu moja au wawili eti ndio sahihi na jumuia nzima ifuate bila kuangalia madhara na faida yake kwa jamii husika. Hakuna mantiki yoyote kuwa kiongozi au raia ambapo mawazo yako yapewe nafasi kwa 100% katika jamii, bila kuhoji kwa umakini. Kama wachunguzi wa mambo , tuliliona hili na ndio maana nilisimama kwenye kikao cha mkutano mkuu kukemea mawazo ya kiwendawazimu kwa ukali bila kujali mtu na nafasi yake kwa niaba ya wale wote wenye nia njema na wana TSU.

Ndugu zangu, napenda muelewe kwamba, nilitoa matamshi hayo ili kila mtanzania mwenye akili timamu aweze kufahamu na kuelewa , ni kitu gani anatakiwa kufuata kwa kuzingatia umuhimu wake katika jamii inayomzunguka.

Napenda mfahamu kuwa, -katika dunia hii, hakuna umasikini mbaya unaowaathiri waliowengi kati yetu kama umasikini wa mawazo, yani mtu unakuwa na fikra Tegemezi. Ndugu zangu watanzania tusiwe tegemezi wa mawazo. Tutafakari kwanza kabla ya kutenda jambo lolote.

Kwa upande wa Uongozi wa TSU na bunge . kwa ujumla , hoja hii ililetwa kwa wanachama mara baada ya kujadiliwa na wajumbe wa vikao husika ndani ya uongozi, maazimio yaliyofikiwa mimi binafsi sijui, ila kimsingi kama wewe kiongozi unategeme nini unapoleta hoja mbele ya mkutano mkuu bila ya maandalizi huku ukiendeleza msimamo wako kwamba huwezi kuendeleza dipromasia. ? kimsingi utakuwa unawaanda wahusika kwa ajili ya movement fulan ambayo wewe binafsi unaona ndio sahihi ifuatwe, ili ujiwekee historia katika maisha yako ya baadae.

Napenda kushauri :- uongozi wa TSU na BUNGE ndio vyombo muhimu katika kujadili hoja nzito zinazoikumba jamii yetu.

Moja- Bunge litumike zaidi katika kuchambua mambo kibusara zaidi bila kukurupuka , kwa kufuata katiba na baada ya hapo kila mwakilishi akutane na wananchi wake katika eneo lake la uwakilishi kwa ajili ya kupitia mchakato mzima wa utekelezaji kwa kura na hata kwa maoni mengine, na baada ya hapo irudishwe bungeni ikajadiliwa na kutolewa taarifa rasmi . baada ya hapo Taarifa rasmi isomwe mbele ya mkutano mkuu na kuhizinishwa na wajumbe wa mkutano mkuu, na utekelezaji wake uanze kazi mara moja. Huo ndio utendaji wa kisomi.

Pili :- uongozi wa TSU, hauna budi kufanya mawasiliano na viongozi wa wanafunzi katika vyuo tofauti hapa urusi ili kwa sauti moja tusimame katika hoja za kimsingi kama wasomi, kumbukeni sisi sote tuko chini ya Udhamini wa serikali yaani BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU .(HSLB).

Huo ndio uongozi wa kisayansi na kisomi zaidi, sio kundi Fulani la wanafunzi ndio lionekane kuwa wasemaji wa wengine. Tukifanya hivyo tutakuwa tumepiga hatua katika kujitambua sisi kama viongozi wa taifa letu kwa kujenga hoja za kimaendeleo.

Tatu:- dipromasia ni sehemu ya uongozi wowote , TSU iko madarakani kidemokrasia , sio kijeshi/kidikteta, sasa kama tumeipa nafasi demokrasia itutawale basi hatuna budi kuipa dipromasia nafasi yake ikiwa ni sehemu tu ya utendaji kazi wa demokrasia.

Kiongozi huwezi kuwa na busara kama hufuati dipromasia katika kutatua matatizo ya jamii yako. Naomba tuelewane hivyo.

Kwa upande wa wanafunzi hapa chuoni:- Tusiwe na tafsiri mbovu za kimaisha.tujaribu kuwa watu wa kuchunguza mambo , tusijenge hoja au kuendeleza mambo ambayo hayatatusaidia kamwe katika ufaninisi wetu kama jumuia.

Nasema hivi:-uchaguzi wa TSU ulimalizika tangu 29 june 2008 , na uongozi uko madarakani kwa kufuata misingi ya katiba. Kwa hiyo tuache marumbano ya fikra kwa ku-refer uchaguzi .Hiki ni kipindi cha utekelezaji tu kwa yale yaliyo mema.

Nayasema haya kwa kila mtu , aweze kuelewa na kutambua umuhimu wake hapa chuoni. Najua mengi yamesemwa , yameandikwa na mengine makubwa zaidi ya hayo yatasemwa na kuandikwa na kujadiliwa kimakundi kuhusu mtu Fulani na maisha yake hapa chuoni. Ila tujiulize kile unachoandika au kuteta kina chembe ya manufaa katika ustawi wa jumuia yetu? Au unatumia uwanja huo kueleza fikra zako potofu na uwezo wako mdogo wa kuchambua mambo yanayoihusu jamii yako. Ndugu zangu , tusijengeane chuki binafsi kwa kivuli cha jina la mwenzako. Mambo yanayoendelea katika mitandao hayajengi bali yanabomoa yale mema tunayaanza na kusambaratisha kabisa thamani ya mtanzania kama msomi ndani na nje ya Urusi. Tuache mawazo ya kiwendawazimu. Tujenge hoja yakinifu kwa manufaa yetu.

Mmiliki wa blog Mr Assenga BT, alijenga hoja ili watu watathimini kwanza huko tunakokwenda , cha kushangaza koments za hoja hizo zinamlenga mtu baki,kashfa na mambo mengi yameandikwa, . wasomi wenzangu fahamuni kuwa HESHIMA NA BUSARA, havinunuliwi dukani, ni vitu ambavyo vinakwenda sambamba na status pamoja na umri wako katika jamii inayokuzunguka- Naomba mnielewe hivyo! Sio kukurupuka na koment za kiwendawazim katka swala tete tulilonalo.

Matatizo ya pesa ni yetu sote, si kweli kwamba watu Fulani miongoni mwetu wanafurahia hali tulionayo, sisi sote inatakiwa tuwe pamoja katika kupambana na hali hii, kwa namna yoyote, lakini yote haya yatafanikiwa ikiwa tutaipa busara mkondo wake.

Mwisho:-ndugu zangu , tujari na kuthamini private ya mtu binafsi . kama una tatizo na mhusika ni vema na haki ukamuona mhusika mwenyewe, sio majungu yameyoshena siasa zaidi, “ tutumie sayansi zaidi katika kujenga hoja”

Kwa mara nyingine tena nawapongeza viongozi wote halali wa TSU chini ya Mwenyekiti Bw. Kanyathare B.E na pia spika wa bunge letu tukufu la jumuia yetu Bw Swilla livingstone(mbunge) kwa kazi nzuri mnaondelea nayo ya kuijenga jumuia yetu tukufu ili wanajumuia waweze kujitambua wanakokwenda kwa manufaa ya Taifa letu tukufu la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Kama una tatizo au maoni /hoja yoyote, usiogope kuwasiliana nami kwa anuani yangu hapa chini.

Aksanteni sana,:- na Mwenyezi MUNGU AWABARIKI

BAKUNDA chrispin D.

Co-chairman of UV-CCM-Moscow(organized committee member CCM-moscow)

Former President of TSU-lumumba university .

Faculty of Engineering.

Department of Oil and Gas technology

Contact:- block 10, room 1417a

Email: chrissba502@yahoo.co.uk

Mobile : +79264817550

+79067416441

Nakala! Mwenyekiti wa TSU- lumumba university

Spika wa bunge la wanafunzi

Mmiliki wa blog ya jamii bwana Assenga BT .

..............15 September 2008............

..................................................... .

Tags:

8 comments

  1. Anonymous says:

    hii ndio busala. na hawa ndio watu wenye hekima na maono. basi tutumie busala hii katika kuelewa na mambo mengine. sio kujadili ndani wa watu, mara leo kalala da demu mwingine, mara kala ugali na picha ya samaki, yote hayo yanakuhusu? weweeeeeeee.....macho kama paka mwizi

  2. Anonymous says:

    Umeanza vizuri kujisafisha. Ila fuata kwa makini kilichoandikwa na wadau kisha jikane nafsi yako ili upate nafasi ya kujichunguza kwa ufasaha kama umeonewa au umesaidiwa kutokana na madongo yote yaliyoelekezwa kwako. Na baada ya hapo ujitahidi kuitambua hadhira unayoipatia mawazo yako, manake jinsi ulivyojieleza kwenye huo mkutano ni kisiasa zaidi (Mbaya zaidi ulitumia maneno ya Bw. Nchimbi na wala siyo kwa msaada wa akili yako kufikiri bali kunakili) na ni rahisi sana mtu asiyeipenda siasa kuboreka au kukereka na hayo maneno (Hivyo usimshangae mtu aliyekukasirikia kwa kumtukana) as the matter of fact TSU siyo chama cha siasa wala siyo mahali pa kupractise siasa. ZIngatia ukweli kuwa siyo wote wanaipenda siasa, kisha uelewe kuwa siyo wote wanaoipenda siasa wanaiweza/wanaijua siasa. Rejea kauli yako: "Kwenye msafara wa Mamba Kenge pia wamo" unaweza kuwa mpenzi mkubwa wa siasa lakini huna kipaji wala uwezo wa kuwa mwanasiasa.. Im praying for you not to be one of those Kenge's in your Political ambition..

    Amini kuwa Ndoto zako zote zinaweza kuwa kweli kama tu ukiwa na lengo pamoja na mikakati thabiti kisha ukapata Baraka za Jamii inayokuzunguka. Zingatia kuto-kukera/kudhalilisha/kukejeli/kupuuza/kujigonga/kujipendekeza kwa/kujisifu/kujionesha kwa/kusimanga.... mtu/watu eti kisa unataka kujijengea umaarufu/heshima. Simamia ukweli daima na heshimu mawazo na mtazamo wako milele kisha tumia akili yako kujenga hoja siku zote kwani hiyo itakusaidia kujiepusha na migogoro isiyo na lazima kutokana na ukweli kuwa kukariri ni rahisi sana kupotosha maana uliyokusudia kwa kuwa akili yako inakuwa haijafikiria deep down kuhusu mtazamo uliou-copy na kuu-paste kichwani kisha kuutoa mzima mzima.

    Otherwise All the Best.

    mtanashati@yahoo.com

  3. Anonymous says:

    mmh we bwana mtu wa ajabu sana hata nashindwa kukudefine.bado upo tuu?

  4. Anonymous says:

    watu wanashauri wakutoe ktk CCM ndio utatulia.maana kuna habari kuwa kuna watu 2 hawatakiwi ktk CCM ili wanachama wengine wajiunge kwa wingi,wewe bakunda ni mmojawapo.sijui unalifikiriaje hilo?ila mi nakushauri ubaki siasa unaiweza kama kwagilwa.

  5. Anonymous says:

    MASELAAAAA MMEONAAAAAAAAAA!!!
    MAMBO KAMA HAYO NDO MAHALI PAKE. HAKUNA KUMUOGOPA MTU BABAKE, MAMBO YOTE HADHARINI NA KWA KUJIAMINI ZAIDI, SAFI SANA GENERAL BAKUNDA:)))))))))
    big up sana, general bakunda, hayo ndo mambo, ulikemea kwenye mkutano na bado unaendelea kukandamiza kinoma!
    hapo nimekubali, hao wanaendele kuteta na hoja zao, ni viboko tu , achana nao, mambo yote umeyaweka hadharani, sio huyo mtanashat(kama anavyojiita)bado anaweweseka na hoja zake za kiwendawazim, wewe mtanashati kama una ubavu na pumzi ya kutosha JENGA HOJA NA WEKA HADHARANI, kama alivyofanya general kwenye mkutano na kwenye mtandao,
    huo ndio usomi, na uelewaji wa mambo , unapokula vizuri, na unaishi vizuri ni lazima utakuwa na hoja za kimsingi ambazo anazitoa kwenye jamii bila woga, kama general alivyofanya.
    general endeleza libeneke la kurekebisha tabia za watu hapa chuon hasa wale wenye hoja za kiwendawazimu
    general , tuko pamoja! BIG UP SANA

  6. Anonymous says:

    NYIE WOTE MNAJIFUNZA SIASA,SIASA SIO NZURI, BORA MNGETUMIA MUDA WENU KUJADILI MAMBO YA KISAYANSI,TEKINOLOGIA NA KIUCHUMI ILI TUWEZE KUTATUA TATIZO SUGU LA KIUMASIKINI LINALOLIKUMBA TAIFA LETU AMBALO LINA VIONGOZI WENYE SURA KAMA HAWA TULIONAO NDANI YA TSU,WANAJIFUNZA TU KUONGEA KAMA VIONGOZI FULANI LAKINI HAWAJUI CHA KUFANYA ILI MAENDELEO YAPATIKANE,NAOMBA MUWE KAMA WANA SAYANSI KWANI WAO HAWATUMII MANENE TU BALI HUTAFUTA SOLUTION KWA KUFANYA PRACTICAL ,,MASKINI NCHI YETU MIAKA KIBAO YA UHURU IKIONGOZWA NA CHAMA KILEKILE LAKINI BADO MASKINI,,TUBADILIKANI JAMANI TUSILIENDELEZE KILE CHAMA KWANZA MJINA WAKE MMBAYA NA UNIFORM ZAKE ZINA RANGI MBAYA KINATIA KICHEFUCHEFU,,TUAMKE WATANZANIA KWA NIABA YA NCHI YETU NA VIZAZI VIJAVYO,,NI SOOO HATA KUTAJA UMETOKEA TANZANIA))))

  7. Anonymous says:

    bakunda kaishiwa.hana jipya.UNALO BABUUU,LIMEKUGANDAAAAAAAAAAAAAAAAAA/

  8. Anonymous says:

    unatisha

Post a Comment