Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - MANOARI YA KIVITA YA RUSSIA IKO NJIANI KUELEKEA PWANI YA SOMALI KUPAMBAMBA NA MAHARAMIA.

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Maharamia wadai dola milioni 35.
Maharamia nje ya pwani ya Somalia.
Maharamia wa Somalia wadai mamilioni ya dola.
Maharamia wanaoishilia meli ya Ukraine nje ya pwani ya Somalia wamerudia madai yao walipwe dola milioni 35 waweze kuiachilia pamoja na mabaharia wake.

Mapema maharamia hao wametoa onyo dhidi ya jaribio lolote la kuwaokoa mabaharia hao au shehena ya mizigo iliyobebwa na meli hiyo MV Faina, vikiwemo vifaru vya kivita 33 vya jeshi la Kenya.

Katika miezi ya karibuni maharamia hao wamekuwa wakiteka meli nyingi zinazopita nje ya pwani ya Somalia.

Manowari ya kivita ya Urusi iko njiani kuelekea eneo la Afrika Mashariki na Marekani inachunguza kinachoendelea katika eneo hilo.

Msemaji wa maharamia hao aliyejitambulisha kwa jina la Jalal Jama Ali, ameuambia mtandao mmoja wa Kisomali, kundi lake limejiandaa kwa mazungumzo na serikali ya Kenya, lakini hawataiachilia meli hiyo hadi watakapolipwa fedha hizo.

Tags:

0 comments

Post a Comment