Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Skendo ya Ngono

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Klabu ya Soka ya Bongo Movie, inayoundwa na mastaa na wadau wa filamu, imekumbwa na skendo ya ngono baada ya ujumbe mfupi wa maneno kusambazwa kwa watu mbalimbali ukionesha uchafu unaofanywa na wacheza sinema hao, Amani linathubutu kufunguka bila woga.


Ujumbe huo uliopenyezwa kwenye simu za wadau wa tasnia hiyo wiki hii unasomeka kuwa, wasanii hao wakiwa Rocky City (Mwanza) siku chache zilizopita kwa ajili ya mechi dhidi ya wanahabari wa mkoa huo, walidaiwa kufanya mambo yaliyo kinyume na maadili ya Kitanzania.


Ujumbe huo ambao Amani limetumiwa zaidi ya mara kumi unakwenda mbali zaidi na kuwatuhumu vigogo wawili (majina tunayahifadhi) wanaofanya kazi ya kuwanadi wasanii wa kike kwa ‘mapedeshee’ kwa  lengo la kujipatia fedha haramu.

Ujumbe huo ulidai kuwa, kila wasanii hao wanaposafiri kwa ajili ya michezo ya hisani katika jamii, kunakuwa na waunganishaji wanaokamilisha mchongo huo.

Wasanii waliokuwa kwenye safari hiyo ni pamoja na Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Wema Abraham Sepetu, Jacqueline Wolper, Steve Mangere ‘Nyerere’,  Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Single Mtambalike ‘Rich’, Jacob Steven ‘JB’, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Hartmann Mbilinyi, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven Kanumba.

Ujumbe huo unadai kuwa, msanii Snura Antony Mushi alikuwa mmoja wa wasanii wa kike waliokumbana na kashikashi wakiwa Mwanza hadi kufikia hatua ya kutafuta pa kulala huku akitahadharisha kuwa ana mtoto mdogo.
Pia ujumbe huo unamtaja mheshimiwa mbunge (jina tunalo) ambaye alishiriki uchafu huo wa kuwanyemelea mastaa hao wa kike lakini akaangukia pua.

Baada ya ujumbe huo kusambazwa, Amani lilifanya jitihada za kuzungumza na watajwa ambapo kila mmoja alikuwa na lake la kusema:

SNURA:
“Siwezi kuzungumza lolote kuhusu skendo hiyo kwa sababu mimi siyo msemaji wa Bongo Movie FC. Ongea na Steven Kanumba, akikuruhusu nitakwambia kila kitu.”

JACK WA CHUZ:
“Siyo Jack mimi, fanyeni uchunguzi wenu, mtagundua ukweli. Mkishafanya uchunguzi, waulizeni viongozi wangu.”
SHILOLE:
“Sijui chochote, muulizeni msemaji ambaye ni Kanumba.”
Katika kutafuta ukweli wa mambo, Amani lilizungumza na Rais wa Bongo Movie FC, Hartmann ambapo alifunguka:

“Hiyo meseji inasambazwa na watu wenye chuki na sisi, hii ni vita, wanalenga kutuchafua, habari hizo siyo za kweli hata kidogo.”

Alipotafutwa Kanumba kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye ni msemaji wa Bongo Movie FC, simu yake ya kiganjani iliita bila majibu na wakati mwingine ilikuwa haipatikani.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu Bongo (TAFF), Simon Mwakifamba alikiri kupokea ujumbe huo na kuahidi kukutana na bodi yake ili kuamua nini cha kufanya kuhusiana na skendo hiyo.

Habari zilizotufikia muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni zilidai kuwa, wasanii hao keshokutwa (Jumamosi) watakuwa na mechi na waheshimiwa wabunge mjini Dodoma.
Kumekuwa na mpasuko kati ya wasanii wa filamu Bongo kwa miezi kadhaa sasa, jambo linaloekea kuwaharibia sifa ya kazi zao za kisanaa.

0 comments

Post a Comment