Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - NBC yasaidia EOTF

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter


Mkuu wa Masoko na mawasiliano wa Benki ya NBC, Mwinda Kiula-Mfugale (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shillingi milioni 18,200,000/- kwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama
Anna Mkapa kwa ajili ya mafunzo ya wanawake wajasiriamali 250 yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika ofisi za EOTF, Dar es Salaam jana. Picha inayofuata wakionyesha mfano wa hundi hiyo.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NBC YAISADIA EOTF KWA KUDHAMINI MAFUNZO YA WANAWAKE WAJASIRIALI 250
DAR ES SALAAM Juni 16, 2011
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi hundi ya shs milioni 18,200,000/- kwa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya siku tatu ya wanawake wajasiriamali 250 kutoka katika mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.


Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi hiyo, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Bi. Mwinda Kiula-Mfugale alisema NBC inajisikia furaha kusaidia mafunzo hayo ya wanawake wajasiriamali kwani yanakwenda sambamba na sera ya benki ya kuongeza ajira.


“Kuongeza ajira ni moja ya nguzo za sera zetu za shughuli za kijamii (CSR) hivyo kwa kuwasaidia wanawake hawa wajasiriamali 250 tutakuwa tumeweka mchango mkubwa katika kuwakomboa wanawake hawa kiuchumi na hivyo kuongeza pato la Taifa”.


Suala la mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ni kitu muhimu kwani licha ya udogo wa mitaji yao ya kibiashara wakipata elimu na mbinu za kufakisha biashara zao zitawasaidia sana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazozipata katika utendaji wao wa kila siku.


“Elimu kuhusu mitaji, elimu kuhusu mikopo, masuala ya masoko, ubora wa bidhaa na ushindani uliopo katika soko la biadhaa wanazozalisha ni nyezo muhimu zitakazowasaidia kufanya biashara zao kwa faida na mafanikio”, aliongeza Bi Mwinda.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa Hundi hiyo Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote, Mama Anna Mkapa aliishukuru NBC kwa mchango wake utakaosaidia kufanikisha semina hiyo ya siku tatu itakayoanza Juni 23 hadi Juni 25 mwaka huu.


Alisema katika mafunzo hayo ya siku tatu wanawake hao wajasiriamali 250 watafundishwa mambo mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, Ugonjwa wa Malaria, HIV/AIDS, Kansa ya Matiti, Masuala ya Benki na Vyama vya Ushirika vya Kuweka na Kukopa (SACCOS).


Hii ni mara nyingine Benki ya NBC inatoa mchango wake katika kusaidia juhudi za wanawake wajasiriamali kujikomboa kiuchumi kama ilivyofanya hivi karibuni kwa kudhamini Tuzo za Wanawake Tanzania (TWAA) kwa kudhamini kitengo cha mjasiriamali bora wa mwaka. Pia, NBC imekuwa kila wakati ikitoa michango mbalimbali kwa vikundi vya wanawake mbali mbali nchini baadhi ikiwa kikundi cha UYAWEKO cha jijini Dar es Salaam na kikundi cha Upendo kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani.

0 comments

Post a Comment