CHAMA cha Mameneja na Wamiliki wa Shule na Vyuo binafsi Tanzania (TAMONGSCO), kimeiomba serikali kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na kutaka mitihani hiyo isahihishwe upya Kikanda ili kila mwanafunzi anayelalamika ameonewa apewe haki yake.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya chama cha NCCR- Mageuzi kuitaka serikali kuangalia upya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa wiki iliyopita na kuisahihisha upya kwa lengo la kufanya achano sanifu (standardisation) ili kuinusuru nchi isiingie kwenye machafuko.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Tamongsco, Benjamin Nkonya alisema utaratibu wa usahihishaji wa mitihani mwaka huu, haukuwa wa kawaida na ulichukua muda mfupi kwa sababu bajeti ya Baraza la Mitihani ilikuwa finyu.
“Bajeti hiyo ilikuwa finyu kwani vyanzo vyake vya mapato vimepungua baada ya serikali kuondoa ada ya mitihani kwa shule za Serikali na kufanya baraza hilo liwe na uwezo mdogo wa kusimamia kazi ngumu ya kusahihisha mitihani ya nchi nzima ya watahiniwa zaidi ya 117,000,” alidai.
Alidai muda mfupi wa wiki moja uliotolewa kwa ajili ya usahihishaji mwaka huu ni tofauti na miaka mingine ambapo hutumika wiki tatu hadi nne jambo linalotia mashaka kama karatasi za watahiniwa wote zilipitiwa vizuri.
“Kasoro nyingine iliyopo nje ya uwezo wa watahiniwa ni migomo ya walimu kuhusu madai yao kwa serikali ambayo ilipunguza morali ya kazi na wakashindwa kuwajibika ipasavyo katika kufundisha na kumaliza mihutasari ya masomo husika,” alisema.
Alisema taifa limegharamia vijana hao kwa kipindi cha mika 11 na kuwaacha na hasara na kwamba Tamongsco inaamini vijana hao ambao ni nusu ya watahiniwa wote sio wajinga kiasi hicho cha kuwaacha bila kuwaendeleza kwa kigezo cha kushindwa mtihani.

0 comments