MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wameanzisha mchakato rasmi wa kurejesha mali za umma yakiwemo majengo na viwanja vinavyodaiwa kumilikishwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), bila ridhaa ya wananchi.
Mali hizo ni kiwanja chenye hati namba 056038/94 cha ukubwa wa futi za mraba 18,790 zilipo ofisi za CCM Moshi Mjini na eneo la hekari 2.7 lenye hati namba 15686 linalotumiwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa.
Katika hatua za awali, madiwani 24 wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, waliwasilisha kizuizi cha kisheria (caveat) ili kuzuia mtu yeyote au taasisi kuhamisha umiliki wa maeneo hayo mawili.
Nyaraka mbalimbali ambazo Mwananchi inazo, zinaonyesha kuwa licha ya madiwani wa CCM kuridhia mali hizo za umma zimilikishwe CCM, bado hati za umiliki zinasomeka ni mali ya Halmashauri ya Mji wa Moshi.
Kutokana na azimio hilo la madiwani lililofikiwa baada ya kupigwa kura na wingi wa kura, Baraza la Madiwani katika kikao chake mwaka 2006, kiliridhia eneo lote la Vijana lenye maduka na makao makuu ya UVCCM mkoa, wapewe Umoja huo.
Halmashauri ya Moshi inaundwa na madiwani 21 wa kuchaguliwa; 17 kutoka Chadema na madiwani wanne kutoka CCM. Idadi hii haijumuishi madiwani wa viti maalumu kutoka vyama hivyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kuweka kuzuizi hicho Ofisi ya Ardhi Kanda ya Kaskazini, madiwani hao wa Chadema walidai mali hizo ni za umma wa wakazi wa Moshi zilizokuwa zikichukuliwa kimabavu na CCM.
“Baada ya kupata taarifa za kiintelijensia kwamba CCM wanahaha kubadili umiliki wa mali hizo tumeamua kuchukua hatua kuzuia kila aina ya uharamia huo,”alisema Abdulrahman Shariff wakati akisoma tamko hilo la madiwani.
Shariff ambaye ni diwani wa Kata ya Bondeni na Katibu wa Madiwani wa Chadema, alifafanua kuwa hatua hiyo ina nia ya kufanikisha ukombozi wa mali za Manispaa ya Moshi na kuokoa mamilioni ya fedha za umma.
Madiwani hao wamedai kuwa wastani wa Sh100 milioni kwa mwaka ambazo ni kodi wanayotozwa wafanyabiashara katika eneo la Vijana, zimekuwa zikiingia UVCCM badala ya kuingia Manispaa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Shariff alisisitiza kuwa CCM kitatakiwa kuilipa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kodi ya pango kwa miaka yote ambayo imekuwa ikitumia jengo la Halmashauri lililopo kiwanja namba 056038/94 karibu na mahakama ya mkoa.
Kwa mujibu wa Shariff, hatua hiyo haina lengo la kumkomoa mtu, chama, taasisi yeyote, bali wanafanya hivyo kwa mujibu wa kanuni na katiba ya nchi.
Hata hivyo, madiwani hao wametahadharisha watendaji wa Serikali kutofanya jambo lolote la kughushi nyaraka ikiwamo kurudisha nyuma tarehe kwa kuwa tayari walishakamata nyaraka zote kuhusiana na umiliki wa maeneo hayo.
Viongozi wa CCM Manispaa ya Moshi na wale wa UVCCM mkoa jana hawakuwa tayari kuzungumzia sakata hilo walipohojiwa na Mwananchi zaidi ya kusisitiza kuwa mali hizo ni zao na wanafuatilia jambo hilo kwa umakini mkubwa.
Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini, Godfrey Mwangamilo alisema jana kuwa ana uhakika mali hizo ni za CCM na UVCCM na kwamba madiwani hao wa Chadema wamekurupuka bila kufanya utafiti wa kutosha.
Mwangamilo alifafanua kuwa madiwani hao hawana haki ya kisheria kulalamika kwa kuwa wamiliki wa eneo hilo ambao ni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi hawajalalamika kokote kuhusu kuhamishwa kwa umiliki wa maeneo hayo.
Katibu Mwenezi wa CCM Manispaa ya Moshi, Bakari Mwacha ambaye awali alidai kuwa si msemaji wa chama, baadaye alifafanua kuwa mambo yanayotokea sasa walijua yangetokea hivyo wamejiandaa kukabiliana nayo.
Katibu wa UVCCM Mkoa Kilimanjaro, Yasin Lema aliliambia Mwananchi kuwa asingeweza kuingia kwa undani kuzungumzia suala hilo zaidi ya kusisitiza kuwa eneo linalozungumziwa ni mali halali ya jumuiya hiyo ya CCM.
Ingawa Katibu huyo alikataa kuingia kwa undani, lakini habari zisizo rasmi zinadai kuwa UVCCM waliuziwa eneo hilo kwa Sh11 milioni licha ya umoja huo nao kuingiza mamilioni ya shilingi kwa mwezi kama kodi kwa wafanyabiashara.
Tukio linaloikumba CCM hivi sasa liliwahi kuikumba tena Moshi Vijijini baada ya Halmashauri hiyo kuwa chini ya Tanzania Labour Party (TLP) ambapo ilibainika ofisi iliyokuwa ikitumiwa na chama hicho ilikuwa mali ya halmashauri.
Baada ya kufukuzwa katika jengo hilo walilolitumia miaka nenda rudi, CCM Moshi Vijijini iliamua kujenga jengo lake karibu na kituo cha mafuta kinachomilikiwa na mfanyabiashara wa Moshi na Arusha, James Selengia.

0 comments