Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Uongozi wa KIIMLA bARANI aFRIKA UNAYOYOMA TARATIIIIBU

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Mubarak aanza kusalimu amri Misri
WAKATI maandamano makubwa ya watu milioni moja yakiendelea katikati ya Jiji la Cairo nchini hapa, Rais Hosni Mubarak, ametoa msimamo unaoashiria kuwa ameanza kusalimu amri baada ya shinikizo hilo la nguvu ya umma linalomtaka atoke madarakani.
Rais huyo akihutubia taifa kupitia televisheni juzi alisema hatagombea tena urais Septemba mwaka huu.
Ingawa alisema ataendelea kuwa madarakani hadi amalize muda wake mwezi Septemba, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema tayari kauli ya kusema “sitagombea tena” inaashiria ameshaanza kusalimu amri na kwamba anachojaribu kufanya sasa ni kupima tu upepo wa kisiasa iwapo waandamanaji hao watatulia baada ya hotuba yake hiyo.
Wanasema iwapo maandamano hayo yataendelea kwa siku chache zaidi, upo uwezekano kwa rais huyo kuachia madaraka kabla ya kumaliza muda wake wa urais.
Kwa upande wake, Rais wa Marekani Barack Obama, amemtaka kufanya mageuzi ya uongozi haraka iwezekanavyo.
“Kwa siku kadhaa tumeona na tumesikia hali ya mambo inavyoendelea katika nchi ya Misri yenye historia kubwa…mabadiliko mapya ya uongozi lazima yaanze sasa,” amekaririwa rais Obama baada ya kuongea na Mubarak kwa simu.
Kiongozi huyo wa Marekani amesema lazima Misri ifanye uchaguzi huru na wa haki.
Katika maelezo yake baada ya hotuba hiyo ya Mubarak, Rais Obama amesema Marekani itakuwa na furaha kwa kutoa ushirikiano kwa nchi hiyo wakati wa mabadiliko ya utawala.
Rais Obama ameonekana kwa kiasi kikubwa kuwapongeza waandamanaji pamoja na majeshi ambao baadaye walikuwa upande wa waandamanaji hao.
Taarifa zinasema baada ya Mubarak kutoa kauli hizo, baadhi ya waandamanaji walionekana kukubali ahadi hizo, lakini wengine waliendelea kupinga huku wakisema: “Hatutaondoka! Yeye ndiye ataondoka!”
Rais huyo amejaribu kutuliza ghasia kwa kuahidi mabadiliko ya kisiasa na akamwagiza Waziri Mkuu mpya, Ahmed Shafiq, kuharakisha mabadiliko ya kidemokrasia ili kubuni nafasi mpya za kazi.
Lakini wachambuzi wa mambo wanasema mabadiliko pekee yatakayokubalika na waandamanaji ni Rais Mubarak kuondoka madarakani.
Tags:

0 comments

Post a Comment