Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unatarajia kutumia Sh400 bilioni kuzalisha megawati 300 za umeme na kuziingiza katika gridi ya taifa, ifikapo Desemba mwaka huu.
Hatua hiyo, ina lengo la kusaidia kuondoa matatizo ya umeme yanayoikumba nchi kwa sasa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC), Zitto Kabwe aliimbia Mwananchi jana kuwa, mtaalamu mshauri wa utekelezaji wa mradi huo, amemaliza upembuzi yakinifu na kwamba mabilioni hayo ni kiwango cha juu cha makadirio ya mradi huo.
"Jumamosi wiki hii, POAC itakutana na NSSF na Stamico pamoja na mtaalamu mshauri ili kupitia na kuujadili na ikiwezekana kuupitisha upembuzi yakinifu wa mradi.
"Mradi unatarajiwa kutumia Sh400 bilioni ikiwa ni makadirio ya juu ya kuzalisha megawati 300 za umeme, utakaoingizwa katika gridi ya taifa ifikapo Desemba mwaka huu,'' alisema Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Mwanzoni mwa mwezi Februari, mwaka huu jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau alisema mfuko wake umemteua mtaalamu mshauri kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, ambao utatokana na makaa ya mawe ya Kiwira.
Pia Dk Dau alitangaza kuwa mfuko wake unaangalia uwezekano wa kutandaza bomba la gesi kutoka Mnazi Bay hadi Dar es Salaam na Mwanza.
“Madhumuni ni kusambaza gesi inayozalishwa hapa nchini katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu,” alisema Dk Dau bila kutoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na mradi huo.
Dk Dau alisema shirika linaendelea kuwekeza rasilimali katika miradi ya muda mfupi na mrefu na kwamba kutoka mwaka 2005/6 hadi 2009/10, uwekezaji wa mfuko uliongezeka kutoka Sh424.89 bilioni hadi Sh1.03 trilioni
Katika hatua nyingine, Oktoba mwaka jana, NSSF ilipandisha pensheni kwa asilimia 52 na kwamba kutokana na mabadiliko hayo, kiwango cha chini cha pensheni kwa wastaafu kimeongezeka kutoka Sh52,000 hadi Sh 80,000 kwa mwezi.

0 comments