Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mabomu ya machozi yarushwa Dar

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter  JIJINI Dar es Salaam polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya maelfu ya wananchi waliokuwa wakifanya maandamano ya kupinga matokeo ya udiwani kata ya Tandika.

Vurugu za aina hiyo pia ziliripotiwa mkoani Kigoma ambako polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika ofisi za halmashauri na kuanza kurusha mawe wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge.

Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea wawili ambao ni Ally Mleh wa Chadema na Peter Selukamba wa CCM.

Vurugu za Tandika zilitokea majira ya alasiri, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya wagombea wa nafasi za Udiwani wa kata ya Tandika ambapo kwa taarifa za awali kutoka kwa msaidizi wa kituo mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Zena Mgaya ameibuka mshindi dhidi ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Bakari Mbegu ambaye ndiye waliokuwa wakichuana vikali.
Tags:

0 comments

Post a Comment