Waziri wa Mambo ya Nje Kenya ajiuzulu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Moses Wetangula amejiuzulu ili kutoa nafasi ya kufanywa uchunguzi kuhusiana na kashfa ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Kenya jijini Tokyo, Japan.
Mwingine aliyejiuzulu kufuatia kashfa hiyo ni katibu wa wizara ya mambo ya nje Thuita Mwangi.
Wote wanashutumiwa kukiuka mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu kuhusu gharama ya jengo hilo.
Kamati ya bunge kuhusu masuala ya nchi za nje na ulinzi, iliwasilisha taarifa bungeni ikipendekeza waziri Moses Wetangula na katibu huyo wajiuzulu, kufuatia sakata hiyo inayokisiwa kuigharimu serikali ya Kenya dola milioni 13.5. Pia kumekuwa na kashfa ya kupotea fedha katika ubalozi wa Kenya ncini Misri, Nigeria, Pakistan na Ubelgiji
Siku ya Jumanne kulikuwa na mjadala mkali ndani ya Bunge la Kenya kuhusiana na ripoti hiyo.
Bw Wetangula amekanusha tuhuma zote hizo. Tuhuma za hivi sasa za ufisadi ndio zinaonekana nzito kugusa kiongozi mwenye dhamana kubwa serikalini mwandamizi.
0 comments