IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Wafanyakazi wakiandamana mjini Marseille.Paris.
Safari za anga, reli na barabara zimeendelea kuvurugika nchini Ufaransa jana jumatano, ikiwa ni siku ya saba ya migomo na maandamano.
Safari za anga , treni na barabara zimeendelea kuvurugika nchini Ufaransa jana Jumatano, ikiwa ni siku ya saba ya maandamano pamoja na hatua ya vyama vya wafanyakazi kufanya migomo dhidi ya mipango ya serikali kupandisha umri wa wastani wa kustaafu kufikia miaka 62. Baada ya tahadhari ya uharibifu wa muda mrefu wa uchumi nchini humo, rais Nicolas Sarkozy ameamuru polisi kuondoa vizuwizi vyote katika mabohari ya kuhifadhia mafuta, hatua ambayo imesababisha kufungwa kwa karibu theluthi ya vituo vya kuuzia mafuta. Waziri wa mambo ya ndani Brice Hortefeux ameidhinisha hatua kali dhidi ya watu wanaogoma. Watu waliofanya ghasia wamechoma moto magari na kupora vitu madukani katika miji kadha nchini ufaransa jana Jumatano. Polisi wameripoti kuwa wamewakamata kiasi watu 1,500 tangu maandamano kuwa ya ghasia.
Sarkozy aapa kuzima ghasia
PARIS
Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amelaani vikali ghasia zilizofanywa kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini humo Lyon na waandamanaji wanaoipinga mipango ya serikali ya mageuzi ya pensheni.
Amewaita waandamanaji hao kuwa ni watu wakorofi na wasiokubalika, na kusisitiza kuwa serikali itapambana nao vikali. Lakini Charles Foulard kutoka muungano wa vyama avya wafanyakazi nchini humo amelaani hatua ya serikali kutumia nguvu.
Maandamanao ya kupinga mipango hiyo kwa sehemu kubwa yamekuwa yakifanyika kwa amani, isipokuwa katika mji huo wa Lyon na kitongoji cha Nanterre kilicho nje kidogo ya Paris ambako wanafunzi walipambana na askari wa kutuliza ghasia.
Baraza la seneti la Ufaransa linatarajiwa kupiga kura kuuridhia au kuukataa mpango huo wa serikali unaotaka kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 60 hadi 62. Vyama vya wafanyakazi vimetangaza kuendelea na mgomo wake kushinikiza kutopitishwa kwa mpango huo.
You Are Here: Home - - Migomo yaendelea Ufaransa kwa siku ya Saba mfululizo. Du! Kama na Ulaya Wanagoma......!!!!!!
0 comments