Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Gari la Chenge lagonga tena, laua

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi mkoani Shinyanga (CCM), Andrew Chenge
Zulfa Mfinanga, Shinyanga na Ramadhan Semtawa, Dar
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi mkoani Shinyanga (CCM), Andrew Chenge ameingia matatani tena baada ya gari lake kudaiwa kumgonga mwendesha pikipiki na kusababisha kifo wakati akitoka kwenye kampeni.Tukio hilo limetokea wakati mwanasheria huyo wa zamani akiendelea na kesi ya mashtaka mawili ya kuendesha kizembe na kugonga pikipiki ya matairi matatu na kusababisha vifo vya watu wawili na jingine la kuendesha gari ambalo bima yake ilishaisha.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa katika ajali ya jana waziri huyo wa zamani wa Miundombini hakuwa akiendesha gari hilo, bali alikuwa ndani.

Habari zilizopatikana jana kutoka wilayani Bariadi zimeeleza kuwa Chenge akiwa anatokea Kijiji cha Namisagusa na Kilalo alikokuwa na mkutano wa kampeni kuelekea mjini Bariadi, alipata ajali hiyo katika Kijiji cha Mbiti kilicho Kata ya Mhango, Tarafa ya Ntunzu.

“Hii ajali imetokea majira ya saa 1:00 usiku, Chenge baada ya kuona gari lake limegonga alishuka na kuhamia katika gari jingine na kuondoka eneo hilo. Wananchi walipofika hapo walilizuia gari hilo, lakini baadaye wakatimuliwa na polisi ambao waliliondoa gari hilo,” alieleza Patrick Liyuba mmoja wa wananchi wanaodai kushuhudia ajali hiyo.

Chenge mwenyewe alipoulizwa kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake, alianza kutoa maneno makali akisema ''andikeni umbea wenu kama mnavyotaka''.

''Sitaki umbea wenu. Niko kwenye jukwaa naomba kura kwa wananchi, ninyi mnaniambia umbea wenu. Tumeshawachoka na umbea wenu mnaoandika kila siku,'' alisema waziri huyo wa zamani wa Afrika Mashariki.   
Mgombea huyo ubunge alihoji: ''Kwani polisi wamesameje.'' 

''Kama wenyewe wenye mamlaka ya kusema wameshasema, mnanipigia mimi ili iweje. Muda wangu ni muhimu sana kuliko kusikiliza umbea wenu wa magazeti, tumewachoka kuwasikiliza, muulizeni huyo aliyewatumia.''

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi alikanusha kuhusika kwa Chenge na kudai kuwa mwendesha pikipiki huyo alipinduka mwenyewe kutokana na mwendo mkali na hivyo kusababisha kifo chake.

Kamanda Siasi alidai kwamba pikipiki hiyo aina ya SUNLG iliyokuwa ikiendeshwa na Penga Machunga, 30, mkazi wa Gamboshi ilipinduka na kusababisha kifo chake papo hapo.

“Ni kweli kwa mujibu wa taarifa za maofisa wangu huko wilayani Bariadi wameripoti kuwepo kwa ajali hiyo ya pikipiki, lakini kama inahusisha gari la Chenge au la nani, basi naomba wananchi ambao wameshuhudia watoe taarifa hizo na sisi tutachunguza na kubaini ukweli,” alieleza Kamanda Siasi.

Alisema kama kuna watu ambao wanajua kuwepo kwa tukio hilo na wanaweza kutoa maelezo ya kina, wafike kituo cha polisi na kueleza hayo ili jeshi lake liendelee na uchunguzi.

Katika miaka ya karibuni, Chenge ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, amejikuta akikumbwa na mikasa mikubwa kuanzi ule wa kuhojiwa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Uingereza (SFO) iliyokuwa ikichunguza kasfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE Systems.

Katika uchunguzi huo, akaunti moja ya Chenge ilionekana kuwa na kiasi cha S1.2 bilioni, ambazo mbunge huyo wa Bariadi alizielezea kama vijisenti
Tags:

0 comments

Post a Comment