Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Nchi za maziwa makuu zahaha kupata fedha za ukimwi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter NCHI za Maziwa Makuu, zinahitahji zaidi ya Sh 14 bilioni, ili kuendeleza miradi ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.

Miradi ya kupambana na ugonjwa huo katika nchi hizo, ilikuwa inafadhiliwa na Benki ya Dunia na ufadhili huo, unakoma rasmi Desemba.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wakurugenzi wa mamlaka za kupambana na Ukimwi katika nchi hizo, walisema kukoma kwa ufadhili benki hiyo iliyokuwa imetoa zaidi ya Sh20 , kwa kumeibua changamoto kubwa.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Dk Fatuma Mrisho, alisema katika ufadhili wa awali uliodumu kwa miaka mitano iliyopita, Benki ya Dunia, ilisaidia mno utekelezai wa miradi mbalimbali hasa katika maeneo ya mipakani, barabara kuu na kambi za wakimbizi.

"Ni kweli kumalizika wa ufadhili wa Benki ya Dunia katika miradi ya Ukimwi, ni changamoto kwetu kutafuta fedha za kuendeleza miradi hii na kubuni miradi mingine,” alisema Dk Mrisho.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mpango wa Kudhibiti Ukimwi katika Jamhuri wa Kidemokrasia na Kongo, Christian Siboko, alisema maambukizi wa virusi katika maeneo ya mipakani na katika kambi za wakimbiuzi ni makubwa na kwamba kuna umuhimu wa kupata fedha, ili kushughulikia tatizo hilo.

Mapema akifungua mkutano wa Baraza la Mawaziri katika nchi hizo, Waziri wa Afya Profesa, David Mwakyusa, alisema, nchi za maziwa makuu, zina majukumu makubwa ya kuendeleza mikakati ya kukabiliana na Ukimwi.


Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, miradi mingi ilifanyika na imesaidia katika kupunguza maambukizi.
Tags:

0 comments

Post a Comment