IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
New York.
Matamshi ya waziri wa mambo ya kigeni wa Israel Avigdor Lieberman jana yamemkasirisha kiongozi wake pamoja na Wapalestina baada ya kusema katika umoja wa mataifa kuwa itachukua miongo michache kuweza kufikiwa amani ya mashariki ya kati.
Akizungumza katika kikao cha kila mwaka cha baraza kuu la umoja wa mataifa , Lieberman amesema kuwa matatizo ya halisi na ya hisia yaliyomo katika mzozo wa mashariki ya kati pamoja na kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa wahusika yanahitaji suluhisho la muda mrefu ambayo yatachukua miongo kadha.
Matamshi hayo yamesababisha ofisi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu kujiweka mbali nayo na kusababisha ujumbe wa Wapalestina kutoka nje ya kikao hicho wakionyesha kupinga.
Taarifa kutoka ofisi ya Netanyahu mjini Jerusalem , imesema , kuwa waziri mkuu ndie anayeongoza majadiliano ya amani akiwakilisha taifa la Israel. Masuala tofauti juu ya makubaliano ya amani yatajadiliwa na kuamuliwa katika meza ya majadiliano tu na sio vinginevyo.
You Are Here: Home - - Matamshi ya Lieberman yamkasirisha Netanyahu
0 comments