Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, amenukuliwa na vyombo vya habari vya Uturuki akieleza kuwa nchi yake itavunja uhusiano ilio nao na Israeli, iwapo nchi hiyo haitoomba radhi kwa mauaji ya Waturuki 9 katika uvamizi huo, au kuyabali matukeo ya uchunguzi wa tume huru juu ya mkasa huo.
Uturuki imefunga tayari anga yake kwa ndege zote za kijeshi za Israeli. Akijibu juu ya msimamo huo wa Uturuki, afisa mmoja wa Israeli leo alirejelea msimamo wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu aliyesema wiki jana kuwa Israeli katu haito omba msamaha kwa kujitetea.

0 comments