IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Israel imesema haitoiomba radhi Uturuki, kuhusu wanaharakati tisa wa Kituruki waliouawa na Israel walipojaribu kuingia Ukanda wa Gaza, unaozingirwa kijeshi na Israel. Kulingana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Israel inasikitishwa kuhusu vifo hivyo,lakini taifa hilo halitoomba msamaha, kwa kuchukua hatua ya kuwalinda wanajeshi wake.
Matamshi hayo ya Netanyahu yanakuja siku moja baada ya Israel na Uturuki kuthibitisha kwamba waziri wa mambo ya nje wa Uturuki na waziri wa biashara wa Israel walikuwa na mkutano wa siri mjini Brussels Ubelgiji. Msimamo wa Uturuki ni kwamba uhusiano baina ya mataifa hayo mawili hauwezi kuwa kama ulivyokuwa, hadi masharti kadhaa yatakapotimizwa, na mojawapo ni Israel kuomba radhi.
You Are Here: Home - - Israel imesema haitoiomba radhi Uturuki
0 comments