IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, amewasili nchini Georgia, ikiwa hatua ya mwisho ya ziara yake katika Mashariki ya Ulaya na eneo la Milima ya Caucasus. Anafanya mazungumzo ya uhusiano unayoyumba kati ya Georgia na Urusi na matarajio ya Georgia kutaka kujiunga na shirika la NATO.
Ameeleza kwamba Marekani inaiunga mkono jamhuri hiyo ya zamani ya Kisoviet, na akailaumu Urussi kwa kuzikalia Abkhazia na Ossetia ya Kusini- mikoa miwili iliojitenga kutoka Georgia. Bibi Clinton pia alizihimiza Georgia na Azerbaijan kuendeleza marekebisho zaidi ya kidemokrasia na kiuchumi, akisema hayo ni muhimu sana katika kuiunganisha tena nchi hiyo.
Hapo awali, Bibi Clinton alitoa wito kwa Armenia na Azerbaijan kutafuta suluhisho la amani juu ya mzozo wao wa muda mrefu juu ya mpaka katika eneo la Nagorno - Karabach liloko katika milima ya Caucasus.
You Are Here: Home - - Hillary Clinton ziarani Georgia
0 comments