IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Hamad Rashid Mohamed
Ramadhan Semtawa, Dodoma
KAMBI ya upinzani bungeni imetoa bajeti mbala, huku ikirarua bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/11, ikisema ni mbaya na kitanzi cha kujinyonga kwa CCM kwenye uchaguzi wa Oktoba.
Kauli hiyo ya kambi ya upinzani imekuja siku moja baada ya kusomwa bajeti hiyo, huku michango yake bungeni kwa jana ikionekana kupoa hasa kwa wachangiaji kutoka chama tawala.
Akisoma bajeti hiyo mbadala jana, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, alisema: “ Mheshimiwa Spika, bajeti hii ya mwaka huu ni moja ya bajeti mbaya katika historia ya nchi yetu.
“Ni bajeti ambayo itaumiza sekta binafsi inayozalisha mali kwa kuitoza kodi nyingi sana ili kulipia gharama za uendeshaji za serikali sio gharama za maendeleo na wakati huo huo, inaifanya serikali ishindane na sekta binafsi katika kutafuta mikopo kwenye benki za biashara.
“Bajeti hii itaumiza ukuaji wa uchumi na kupelekea uzalishaji kupungua na hata kusababisha watu kukosa ajira au kupunguzwa kazini kwa wingi. Bajeti hii ni bajeti ya kujinyonga kwa chama kinachotawala kwani itaongeza ukali wa maisha kwa wananchi.”
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, bajeti ya serikali imeshindwa kujibu changamoto za umma na inasaidia zaidi wenye nacho kuliko watu masikini.
“Hasira za wananchi hao watazionyesha katika masanduku ya kura mwezi Oktoba mwaka huu na Kambi ya Upinzani inaamini watakuwa na haki ya kufanya hivyo,” alisisitiza Rashid.
Huku akionyesha kushangazwa na ongezeko la fedha za matumizi ya kawaida kuliko ya maendeleo, Rashid alisema serikali haijui hata Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Kambi hiyo imetoa mchanganuo wa bvajeti yake kulingana na vipaumbele ambao ni pamoja na kutengea kilimo asilimia 12 ya bajeti ambayo ni Sh1359.64872.
You Are Here: Home - - Wapinzani: Ni bajeti ya kuinyonga CCM Oktoba
0 comments