Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wagombea sita wajitosa urais Zanzibar, YUMO DK SHEIN, DK BILAL,NAHODHA,KARUME NA SHAMUHUNA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein ambaye anatarajia kuwania nafasi ya Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

 
JUMLA wa wagombea sita akiwemo Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein wanatarajiwa kuchukua fomu za kuwania urais wa Zanzibar keshokutwa  kupitisha Chama Cha Mapinduzi (CCM).Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Uenezi na Itikadi ya CCM Zanzibar iliyosambazwa kwa vyombo vya habari mjini hapa imesema kwamba wagombea hao watachukuwa fomu keshokutwa katika nyakati tofauti.
 
Ratiba inaonyesha kwamba Dk Shein atafika Kisiwandui majira ya saa tisa jioni akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Abeid Karume, Kamishna wa Idara ya Utamaduni Zanzibar, Hamad Bakari Mshindo na Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamuhuna.

Wagombea watarajiwa hao, watatanguliwa na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha na Waziri Kiongozi Mstaafu, Dk Mohammed Gharib Bilal wanaotazamiwa kuwa ni watu wa kwanza kuingia katika jengo la Ofisi Kuu Kisiwandui keshokutwa asubuhi kwa ajili ya kukabidhiwa fomu hizo.

Hata hivyo, kabla ya kuchukua fomu leo hii Dk Bilal anatarajiwa rasmi kutangaza nia ya kujitosa katika kinyang'anyiro hicho cha kugombea urais wa Zanzibar.
 
Naibu Katibu Mkuu wa, Saleh Ramadhan CCM Zanzibar, Ferouz anatarajiwa kuwepo ofisini kwake nyakati za asubuhi Kisiwandui kwa ajili ya kuwakabidhi viongozi hao fomu za kuwania nafasi hiyo ya rais, wajumbe wote watakaotaka kuingia katika kinyanyanyiro hicho.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mwenezi wa Idara hiyo, Vuai Ali Vuai inasema kwamba keshokutwa ni siku ambayo wagombea wa CCM wanaotaka kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar watachukuwa fomu hadi Julai Mosi mwaka huu kama siku ya mwisho ya kurejesha fomu hizo.
 
Katika hatua nyengine, baadhi ya wanachama CCM kutoka mikoa mitano ya Unguja na Pemba wanatarajiwa kumkabidhi fedha taslim Dk Bilal zilizokusanywa na wanachama hao kama mchango wao kwa ajili ya kumtaka achukue fomu za kuwania nafasi hiyo.
 
Aidha, Dk Bilal anatarajiwa kuzugumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View iliopo nje kidogo na Mji Mkongwe wa Zanzibar.
 
Dk Bilal aliwahi kuchukua fomu kumpinga mgombea wa CCM ambaye kwa sasa ni rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika vipindi viwili vya uongozi wake.
 
Hata hivyo, Dk Bilal alishauriwa kuliondoa jina lake kutokana na utaratibu wa chama hicho ni kumuachia kiongozi aliyepo madarakani kumaliza vipindi vyake viwili vya uongozi, lakini alikataa kuondosha jina lake hadi lilipofika Dodoma kwenye vikao vya juu.
Tags:

0 comments

Post a Comment