IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Majeshi ya Israeli yanasema yamechukua udhibiti wa meli ya misaada iliyokuwa ikijaribu kukiuka amri kuinga Ukanda wa Gaza.
Israel imeeleza kuwa wanajeshi wake waliingia katika meli ijulikanayo kama Rachel Corrie ikiwa baharini na hapakuwa na upinzani wowote kutoka kwa watu waliokuwa ndani yake.
Imesema meli hiyo imevutwa kwenda bandari ya Ashdod nchini Israel. Hakujawa na maelezo yoyote kutoka kwa watu waliokuwa katika meli.
Mkasa huo umetokea siku tano baada ya watu tisa kuuawa katika mapambano wakati wanajeshi wa Israel walipovamia meli ya misaada kutoka Uturukki, tukio lililosababisha malalamiko kutoka jamii ya kimataifa.
Israel imesema meli itakapokuwa bandarini hapo itawahoji waliokuwa katika chombo hicho na kisha baada ya kuchambua mizigo na kuridhika haihatarishi usalama itaipeleka Ukanda wa Gaza kwa njia ya gari.
Meli hiyo kutoka Ireland ina wanaharakati watano raia wa Ireland na wengine sita kutoka Malaysia, pamoja na mabaharia.
Israel imeweka kizuizi cha kuingia na kutoka Gaza tangu mwaka 2007, wakati kundi la wanamgambo wa Hamas liliposhinda uchaguzi na kupata mamlaka ya kuongoza Palestina.
You Are Here: Home - - Israel yazuia meli nyingine kuingia Gaza
0 comments