Al Gore wa Marekani atengana na mkewe
Aliyekuwa makamu wa Rais wa Marekani Al Gore na mkewe Tipper wanatengana baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka 40.
Mgombea huyo wa urais kupitia chama cha Democrat mwaka 2000 na mkewe wameandika kwa rafiki zao kupitia barua pepe, "ni uamuzi wa pamoja kutoka sote wawili."
Bw Gore, makamu wa Rais wa Bill Clinton, alishinda tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 2007 kwa shughuli zake za mabadiliko ya hali ya hewa.
Bi Gore ni mwanasheria wa muda mrefu juu ya maswala ya afya ya akili. Wawili hao walioana mwezi Mei 1970.
Faragha
Bw na Bi Gore, ambao wote walizaliwa mjini Washington na kukutana huko huko, wamekuwa wakiishi Tennessee. Wana watoto wanne.
Katika barua pepe waliyotuma kwa rafiki zao na watu wanaomuunga mkono iliyotolewa na mashirika ya habari ya Marekani, wameamua kutengana baada ya "kutafakari kwa muda mrefu na kwa kina."
Wameomba wapewe faragha na hawana nia ya kutoa maelezo zaidi.
0 comments