IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, sasa anatajwa waziwazi na kuhusishwa na mpango wa mapinduzi ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Tanzania Daima Jumatano imeelezwa.
Baadhi ya vyanzo vya habari kutoka ndani ya UVCCM vimeliambia gazeti hili kuwa mtoto huyo ndiye anayevuruga umoja huo.
Ridhiwani, ambaye ni mwanasiasa kinda, lakini kwa kuwa mtoto wa rais anakuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama, anatajwa kuwa kinara wa mkakati mchafu unaolenga kumuengua Mwenyekiti wa umoja huo, Hamad Masauni Yusuf.
Mtoto huyo, ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, anadaiwa kuwa ndiye msukaji wa mkakati wa kumng’oa Masauni katika wadhifa wake.
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam na miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu wa umoja huo waliopo mkoani Iringa, zinaeleza kuwa nyaraka zilizoenea kwenye vyombo vya habari nchini kuhusu kashfa ya Masauni kuhusu tuhuma za kughushi umri wake, zimetokana na kazi ya Ridhiwani.
Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano umebaini kuwa viongozi hao wanabadilishana taarifa nyeti kuhusu mgogoro wa umoja huo na kumtaja Ridhiwani kama mhusika mkuu wa kuupanga na kuutekeleza.
You Are Here: Home - - Ridhiwani Kikwete aivuruga CC
0 comments