Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Babu Seya kukata tena rufaa kortini

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya anatazamiwa kukata tena rufaa kortini ambapo jopo la Mawakili limejipanga kumtetea.
JOPO la Mawakili wanaomtetea mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Papi Kocha, leo linatarajia kuwasilisha maombi ya marejeo ya hukumu iliyotolewa Februari 13, mwaka huu na mahakama ya Rufaa.

Kiongozi wa jopo hilo, Mabere Marando jana alisema wanatarajia kuwasilisha maombi ya marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama ya rufaa kwa sababu iliamuliwa vibaya bila ya kuzingatia sheria iliyopo.

Maombi ya marejeo ya hukumu iliyotolewa Februari 13, mwaka huu na mahakama ya rufaa ni kwa ajili ya kutafuta uwezekano wa kumwachia huru mwanamuziki huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mwanaye Papi Kocha.

Siku hiyo ya hukumu Babu Seya na mwanaye Papi Kocha waliamriwa kuendelea kutumikia kifungo cha maisha jela, lakini mahakama hiyo iliwaacha huru wanaye wengine wawili Nguza Mbangu na Francisi Nguza.

Marando alidai kanuni inasema maombi hayo ya marejeo ya hukumu yataenda mbele ya jopo lilelile la majaji na kuongeza kuwa lakini jaji mkuu ana madaraka ya kuteua majaji wengine wa kusikiliza maombi hayo ya marejeo au kuongeza idadi ya jopo la majaji.

“Jaji mkuu anaruhusiwa kufanya hivyo kwa uwezo wake, hivyo tunamuomba kuongeza jopo la majaji,” alidai Wakili Marando.

Oktoba 2003, Babu Seya na wanae walitiwa mbaroni na polisi na kuhojiwa kisha walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu kwa tuhuma za kuwabaka na kuwalawiti watoto wa kike 10, ambao wote walikuwa ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa iliyoko Sinza, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Babu Seya na wanaye watatu, mwalimu wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka, aliunganishwa katika kesi hiyo.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Addy Lyamuya washtakiwa wote kwa pamoja walisomewa jumla ya mashtaka 23,lakini akaachiwa huru.

Babu Seya na wanaye walikuwa wakikabiliwa na makosa 10 ya kuwabaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na nane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri kama huo.

Mwalimu Ligomboka alisomewa mashtaka mawili ya kumsaidia Babu Seya kutenda makosa ya kubaka na kulawiti kwa kuwaruhusu baadhi ya watoto hao kutoka madarasani.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Aprili na Oktoba 2003 eneo la Sinza kwa Remmy, jijini Dar es Salaama katika nyumba namba 607.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa siku chache baada ya ushahidi kukamilika, kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2004 na jumla ya mashahidi 24 wa upande wa mashtaka waliitwa mahakamani na kutoa ushahidi wao.

Mashahidi hao ni pamoja na watoto waliodaiwa kufanyiwa ukatili huo ambao walidai kuwa watuhumiwa waliwafanyia vitendo hivyo kwa nyakati tofauti.

Upande wa utetezi (washtakiwa), ulipeleka mashahidi wanane kuwatetea wakiwamo washtakiwa wenyewe.

Baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mwisho za pande zote mbili, Juni 25, 2004 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa hukumu.

Katika hukumu hiyo hakimu Lyamuya alitupilia mbali na utetezi wa Babu Seya na wanawe, pamoja na wa mashahidi wao ukawatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wakikabiliwa nayo na kuwahukumu adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.

Hata hivyo, Mwalimu Ligomboka aliachiwa huru baada ya kubainika kuwa hana hatia.

Mbali na adhabu ya kifungo cha maisha jela, pia Hakimu Lyamuya aliwaagiza washtakiwa wote kuwalipa fidia ya Sh2milioni walalamikaji wote(watoto) waliodaiwa kubakwa na kulawitiwa.

Hata hivyo washtakiwa hawakukubaliana na hukumu hiyo pamoja na adhabu hiyo, hivyo mwaka huo huo (2004) kupitia kwa wakili wao aliyekuwa akiwatetea Hubert Nyange walikata rufaa Mahakama Kuu.

Katika rufaa hiyo, Babu Seya na wanawe walikuwa wakipinga hukumu hiyo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na adhabu kwa jumla.
Tags:

0 comments

Post a Comment