You Are Here: Home - - 'Ni vigumu kumpata mwingine kama Baregu UDSM' aliyefukuzwa ka madai ya kuelemea CHADEMA
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MKUU wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, amesema, uamuzi wa chuo hicho kukataa kumuongezea Profesa Mwesiga Baregu mkataba wa kufundisha chuoni hapo unaweza kuwanufaisha watu wengine kwa kuwa ni miongoni mwa maprofesa wazuri Afrika.
Dk Bana ameishauri Serikali ikatafakari upya sheria hiyo iliyosababisha Profesa Baregu asiongezewe mkataba.
Amesema, Sheria hiyo ni mbaya kwa kuwa inamuondoa mtaalam kama Prof Baregu katika ajira kwa vile tu anajihusisha na siasa.
“Na kama sisi hatumuhitaji wenzetu watamchukua. Pia lazima ikumbukwe kwamba itachukua miaka mingi sana kuwapata watu wengine kama Baregu na pengine tusiwapate kabisa
“Nilikuwa nasubiria kwa hamu siku Baregu atakaporudishwa, ningekunywa japo kachupa kamoja ka-Kilimanjaro nijipongeze. Kwa kweli yeye ni profesa mwenye uwezo na sisi wasomi tujitahidi kuupata na kuupitia waraka huo ili tuweze kuhoji.”
“Ni habari mbaya kwangu, Prof. Baregu alikuwa mmoja wa maprofesa wazuri katika idara yangu na mchango wake bado ulikuwa unahitajika. Ni profesa mwenye uwezo mkubwa katika Tanzania na katika Afrika Mashariki kwa upande wa mambo yanayohusu uhusiano wa kimataifa,” alisema Dk Bana.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa,amesema,Profesa Baregu hakuongezewa mkataba ili kumkomoa kutokana na msimamo wake thabiti wa kuwa upinzani.Alitaja msimamo wake ni wa kuikosoa Serikali, kutetea umma, na kuunga mkono Chadema.
Alisema, kamati imelazimika kuamini hivyo kwa kuzingatia hali ya kisiasa nchini wakati uamuzi huo umefanywa kuna uhaba wa wahadhiri waandamizi kama yeye katika chuo hicho.
0 comments