Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - JWTZ sasa yajitosa kudhibiti uharamia

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter YATUMIA MAKOMANDOO KUKAGUA MELI ZINAZOINGIA NA KUTOKA

Patricia Kimelemeta

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limejitosa kwenye shughuli za kudhibiti uharamia unaofanywa katika pwani ya Afrika Mashariki na baadhi ya raia wa kigeni.

Chini ya mpango huo JWTZ sasa inakagua na kusindikiza meli zote zinazoingia na kutoka nchini.

Hayo yalisemwa jana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo, alipokuwa akizungumza katika kikao cha Kamati ya Hesabu za Serikali, kilichofanyika jijini Dar es Salaam .

Luteni jenerali Shimbo alisema hatua hiyo inalenga katika kuhakikisha meli zinazoingia na kutoka nchini zikiwemo za biashara, ziko katika salama.

Alisema hadi sasa usimamizi huo umeonyesha mafanikio ya kuridhisha.

Kwa mujibu wa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ jeshi limeteua makomandoo wa baharini, kufanya kazi za ukaguzi na usimamizi wa meli hizo na kutoa taarifa katika mamlaka zinazohusika.

"Naomba niwahakikishie kuwa tatizo la uharamia katika pwani yetu halitafika kwa sababu tuimejipanga kikamilifu kwa kuweka 'patrol' za mara kwa mara pamoja na ukaguzi wa kila meli inayoingia na kutoka, na katika hilo tumefanikiwa,"alisema Luteni jenerali Shimbo.

Alisema shughuli hizo zinawahusisha pia wadau mbalimbali ikiwemo maofiusa wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na kusisitiza kuwa lengo ni kudhibiti vitendo vya uharamia.

Alisema JWTZ ina rada inayosaidia kwa kiwango kikubwa kuratibu shughuli zinazofanyika baharini zikiwemo za uvuvi na nyinginezo.

Luteni jenerali Shimbo alisema chombo hicho, kimesaidia mno katika kupata taarifa mbalimbali zinazohusu uharamia ndani ya bahari.

Hata hivyo Mnadhimu Mkuu alisema jeshi linakabiliwa na tatizo la vifaa vya kisasa zaidi vya kuliwezesha kufanya shughuli hizo kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyo sasa.

Aliiomba serikali, kuliongezea jeshi fungu la pesa katika bajeti yake ili waweze kununua vifaa vya kisasa ambavyo vitaweza kusaidia kupambana na uharamia kwa kiwango cha juu zaidi.

Mwenyetiki wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo, alisema kati hiyo itashirikiana na ile ya Ulinzi na Usalama, kuishauri serikali, ili iliongezee jeshi bajeti ya kununulia vifaa.
Tags:

0 comments

Post a Comment