You Are Here: Home - - Iringa ndio kidume cha maambukizi ya Ukimwi Tanzania
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Iringa ndio kidume cha maambukizi ya Ukimwi Tanzania
Bado hayajasaidia sana kutokana na takwimu za sasa kwa kuonyesha kwamba maambukizi hayo hivi sasa moto hadi kufikia asilimia 24.5.
Ni yale matumizi makubwa ya fedha ya kupambana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi Mkoani Iringa, bado hayaja pungua yanazidi kupamba moto.
Takwimu za mwaka 2007/2008 zilionyesha kwamba maambukizi ya ukimwi mkoani Iringa, uliokuwa ukiongoza kitaifa yalikuwa asilimia 15.7.
Takwimu hizo za kukatisha tamaa zilitolewa katika kikao maalum cha kupitia utekelezaji wa mkakati mpya wa miaka minne wa Mkoa wa Iringa wa kupambana na ukimwi, kilichofanyika Makambako, wilayani Njombe Mkoani hapa.
Taarifa zilizowasilishwa katika kikao hicho zinaonyesha kuwa, matokeo ya upimaji wa virusi vya Ukimwi kwa hiar, ni i kati ya Julai 2008 hadi Juni 2009.
Na yalionyesha kwamba, mambukizi ya virusi vya ukimwi hivi sasa ni asilimia 24.5 ingawa upimaji huo hauwakilishi sampuli za mkoa mzima.
Takwimu hizo zilimkera Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Aseri Msangi, ambaye alisema inashangaza kuona kwamba kasi ya maambukizi hayo inaongezeka wakati, mkoa na wadau wake wanapata fedha nyingi zaidi kwa ajili ya mapambano yake.
Inakuwaje kadri tunavyotumia fedha nyingi zaidi ndivyo maambukizi yanavyozidi kuongezeka… Kwa nini?.
Oktoba 2008, Mkoa wa Iringa ulizindua mkakati wa miaka minne wa kupambana na ukimwi ambapo hadi Oktoba 2009, Mkoa pamoja na wadau wengine ulitumia Sh. bilioni tatu katika kupambana na maambukizi hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Charles Gishuri pia alionyesha kutoridhishwa na utendaji wa Mkoa na wilaya katika mapambano hayo.
Katika kila dalili zinazoonyesha kuwepo kwa ufisadi wa fedha za ukimwi Mkoani Iringa, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Getrude Mpaka, alitoa taarifa iliyoshtua wengi kwamba tangu achukue wadhifa huo mkoani hapa, hajawahi kupata taarifa yoyote ya maandishi ya Kamati ya Ukimwi ya Mkoa ikieleza jinsi inavyoratibu mapambano dhidi ya janga hilo.
0 comments