Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Hakuna mgogoro CHADEMA asema Mbowe, atofautiana na Mama yake Zitto

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Naibu katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zitto Kabwe ambaye msimamo wake ni kuhakikisha kuwa anamsaidia rafiki yake David Kafulila katika kampeni za ubunge kigoma kusiniMGOGORO unaofukuta ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umechukua sura mpya jana baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kutofautiana kauli na mama wa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, Shida Salumu kuhusu fukuto hilo linalohusisha uongozi wa kitaifa wa chama hicho. Wakati Mbowe huku akijiamini aliwaeleza vijana wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa hakuna mgogoro kabisa ndani ya chama, mama wa Zitto, Salumu alitoa kauli tofauti ya kuutaka uongozi wa chama kumuita mwanawe ili ahojiwe kuhusu kauli zake anazozitoa zinazoashiria kuwepo kwa mgogoro. Kauli ya Mbowe na mama mzazi wa Zitto, walizitoa kwa nyakati tofauti katika Kongamano la Vijana lililoandaliwa na chama hicho walipokuwa wakijibu maswali ya wanafunzi walioshiriki mara baada ya kumaliza kuwasilisha mada mbalimbali kuhusu sera za chama hicho za majimbo kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu. “Ndani ya Chadema hakuna mgogoro, zipo propaganda zinazoenezwa na watu nje ya chama ili kuonesha kwamba ndani hatuelewani, zinatengenezwa kujenga mazingira ya kuhalalisha uwongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uwongo,” alisema Mbowe kujibu moja ya maswali ya vijana hao wa chuo kikuu. “Haiwezekani mgogoro kuwepo usiipasue Halmashauri Kuu ya chama, kilichopo ni uhuru wa kuzungumza unaozingatia demokrasia,” Mbowe aliendelea kutoa ufafanuzi kukana kabisa mgogoro huo.
Tags:

0 comments

Post a Comment