Papa John Paul II (kushoto) akiwa na Mehmet Ali Agca alipomtembelea gerezani mjini Roma.
Mehmet Ali Agca mwenye bastora iliyozungushiwa duara akijiandaa kumshambulia Papa John Paul II.
Papa John Paul II baada ya kupigwa risasi na Mehmet mei 13, 1981 St. Peter's Square mjini Roma.
Papa John Paul II akizungumza na Mehmet alipomtembelea gerezani.
Mtu aliyejaribu kumuua papa John Paul wa Pili yapata miaka ishirini na tisa iliyopita, ataachiliwa huru hii leo kutoka gereza la Uturuki.
Mtu huyo Mehmet Ali Agca ametumika kifungo cha miaka kumi na tisa nchini Italia kwa kumpiga risasi papa John Paul na miaka kumi nyingine nchini Uturuki kwa shitaka la awali la mauaji.
Sababu ya bwana Agca kutaka kumuua papa huyo imebakia kitendawili. Kwanza alisingizia idara ya polisi ya Bulgaria kuwa imemtuma na baadaye akaiambia mahakama kuwa yeye ni masiha mpya.
0 comments