Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kili stars yatinga nusu-fainali Chalenji

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Ngassa aivusha Kili Stars kuivaa sasa kuivaa Rwanda
Mrisho Ngassa wa Taifa Stars na Kilimanjaro Stars sasa anaongoza kwa kufunga jumla ya magoli matano katika mashindano ya chalenji.
*Zanzibar na Uganda hapatoshi leo

Michael Momburi, Nairobi

KILIMANJARO Stars imefuzu kucheza nusu fainali kwa kishindo baada ya kuiadhiri Eritrea kwa mabao 4-0 huku Mrisho Ngassa akiibuka shujaa kwa kupachika mabao matatu peke yake (hat-trick).

Mabao hayo yanamfanya Ngasa kufikisha idadi ya mabao matano katika mechi nne alizocheza na usukani wa ufungaji wa mabao akimpiku Mzambia James Chamanga aliyefunga mabao manne katika michuano ya Kombe la Chalenji ambayo inaingia nusu fainali leo kwa mchezo wa kwanza baina ya Zanzibar Heroes na The Cranes ya Uganda.

Kilimanjaro Stars iliyouanza mchezo huo kwa kasi na kupoteza nafasi nyingi za kufunga walilazimika kusubiri hadi kipindi cha pili pale kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, John Bocco alipotumia vizuri urefu wake kwa kuruka juu na kuunganisha krosi ya beki Shadrack Nsajigwa dakika ya 61.

Winga Ngassa alifungulia karamu yake ya mabao kwa kufunga bao lake la kwanza akitokea upande wa kulia na kupiga krosi iliyokwenda moja kwa moja wavuni.

Nyota huyo wa Tanzania aliyekuwa mwiba mkali kwa ngome ya Eritrea kwa kufanya atakavyo akiwazidi mbio na chenga alifunga bao lake la pili na la tatu kwa Stars dakika 76 kwa shuti akimalizia kazi nzuri ya Bocco.

Ngassa alifunga bao lake la tatu dakika ya 84 baada ya Stars kugongea pasi nyingi kabla ya Mwaipopo kupitisha pasi ya juu iliyomkuta mfungaji huyo aliyempiga chenga kipa Yosief Zeratsion wa Eritrea na kumalizia mpira wavuni.

Hii ni mechi 32 ya kimataifa kwa Ngassa akiwa amefungaa mabao 10, huku Bocco akiwa amefunga bao lake la pili kwa Tanzania katika mechi 8 alizocheza.

Kwa ushindi huo, Kili Stars itachuana na Rwanda iliyoitoa Zimbabwe kwa mabao 4-1

Tags:

0 comments

Post a Comment