Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Glob hii ya jamii imefuatilia kwa ukaribu Mkutano Kati ya Ubalozi wa Tanzaia Moscow Russia na mkuu wa chuo kikuu cha Urafiki Lumumba..

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Kutokana na Notisi ya siku 15 kuwatimua masomo wanafunzi 76 wa Tanzania wanaosoma Chuo Kikuu Cha Urafiki Moacow Russia, Ubalozi wa Tanzania Moscow Russia Ulifanya mkutano na Mkuu wa Chuo hicho siku ya jumanne tarehe 01/12/29 ili kujua hatima ya wanafunzi hao. Katika mkutano huo iliamuliwa kuwa wanafunzi ambao hawakuletewa ada kabisa kwa mwaka wa masomo 208/2009, wanafunzi ambao waliletewa nusu ya fedha za ada na wale ambao ada zao zilikosewa kulipwa na Wizara mwaka wa masomo 2007/2008 watavumiliwa kwa muda hadi matatizo yao yatakapotatuliwa. Aidha wanafunzi ambao walibadilisha kozi kiholela na matokeo yake kukatokea ongezeko la ada baada ya bodi kutuma fedha na wengine wote ambao kwa sababu zao binafsi hawakulipa ada, watatimuliwa masomo ifikapo tarehe 15/12/2009. Taarifa za Kuaminika ziliiambia Globu hii ya jamii kuwa wanafunzi ambao hawakulipa ada hiyo kwa sababu zilizotajwa hapo juu hawazidi 15 ambao watavumiliwa hadi matatizo yao yatakapotatuliwa. Kutokana na mkutano huo maalumu, Uongozi wa chuo umetoa tahadhari kwa wanafunzi wote wanaodaiwa kama ilivyoelezwa hapo juu wakalipe michango hiyo kabla ya tarehe iliyotajwa ili kuepuka usumbufu wa kuja kulipa kwa gharama za mkataba mpya pindi Prikaz (order) kuhusu kutimuliwa chuo itakapokuwa imesainiwa.
Glob hii ya jamii inatoa pole kwa wale ambao kwa sababu za msingi za kimaisha walishindwa kulipa ada hiyo na inawahimiza wale wenye nafasi ya kulipa wakati huu wafanye hivyo ili kueputa usumbufu binafsi na sifa mbaya kwa Taifa.
Na THE THOMCOM Inc. Ask for Quality....
Make The world The Best Place to Live.......
Tags:

15 comments

  1. Anonymous says:

    sasa mr boni kwa wale ambao walibadili cozi kihalali wakatoka cozi ya bei ya chini kwenda ya bei ya juu lakini walibadili kihalali na hawakutumiwa hela ya kuongezea kwenye cozi waliyohamia inakuwaje?

  2. Anonymous says:

    nyie mnaohangaika kubadili kozi kila kukicha kwanini hamuuliz process zinavyotumika kwa viongozi ama ubalozini? nyie mnakurupuka tu hao, hamjui kuwa hii ni busness?chuo hakiwezi kukukataza kubadili coz anajua faida itaingia matokeo unaumia wewe. muwe mnatumia akilia na maarifa sio kuvamia tu mambo kichwakichwa.... hovyooooooooo!

  3. Anonymous says:

    mh na wewe!!!!!!!!!
    we mwenyewe mbona ulibadilisha.

  4. Anonymous says:

    we mzee wa kichaga shimboni bae acha kuwadanganya wenzio,bodi haidaiwi na mwanafunzi yeyote ada ya 2008/2009,kama wamekula wategemee kufukuzwa tu ama walipe walizotumiwa sasa.

  5. Anonymous says:

    ivi jamani kweli watu tuko tofauti.mtu umepewa ada kabisa unakula au kufanyia mambo yako binafsi unajipenda wewe kweli?ukifukuzwa chuo utamlaumu mtu?mimi hata siwaonei huruma mwenzenu maana ni uzembe wenu huo.utakula vp ada mwanafunzi wa chuo mtu mzima wewe.kweli dunia ina mambo.hovooooooooooooooooo!!!!!!!!

  6. Anonymous says:

    kama mtu kala ada kakuombe umsaidie kulipa? au hujui mchuma janga hula na wakwao? kama hudaiwi basi nyamaza sio unatumatuma comment tu hapa kwa vile ushaweza kutumia keybord

  7. Anonymous says:

    wewe assenga kama umeamua juwa mwandishi wa habari basi kua mwandishi na wala usiwe mshabiki manake wewe upo asaftu na hawa wenzetu waliokula ada wapo wengi sasa mabala ya kuongea nao au na chuo wewe unakuwa upande wa chuo wa kuwafukuza tumia akili sio iunashabikia vitu ut hapa .kwanza cheki kuna mtu anadaiwa doa 800 akifukuzwa tiketi ya kumpeleka tanzania ni dola 1000 sasa si uchizi huo? wewe unafanya nini assaftu au unaenda kunywa chai tu huko viongozi tuwasaidieni hawa jamaa hili lakini simaanishi tuwachangie

  8. Anonymous says:

    anony.hakuna kumsaidia mtu hapa nani kawaambia wale ada? hela ilitumwa ili watu walipe sasa wewe unaila unategemea nini?mnalo

  9. Anonymous says:

    poa tufukuzeni kwanza mwisho wa dunia ni 2012 sio mwiso wa dunia in such lakini planet itabidestroyed sasa assenga sijui unashabikia nini

    www.december212012.com/
    najua hamtaamini lakini hii ni kweli na wanascience wameshathibitisha sema hawataki kuitangaza official kwa sababu uchumu wa dunia utayumba .kuhusu ile moovie waliitoa baada ya hizi taarifa so stay tuned..hihihi sisi tunafukuzwa wewe umekula mikate unapata kidploma chako unarudi planet inakuwa destroyed.kwa hiyo msishabikie vitu ut hapa tubuni acheni mipombe misigara mademu uongo wizi hope mmenipata wakuu wadanganyika

  10. Anonymous says:

    hawa watu wote wamesoma hii taarifa wewe kama hujui unafanya nini? unakula mikate tu sio hihihi unasabikia wenzetu waliokula ada mimi nawasifu hawali mikate the end is near
    http://www.december212012.com/believers_list.htm

  11. Anonymous says:

    we sa ivi unatapatapa kalipe hakuna mwishi wa dunia

  12. Anonymous says:

    hhahahhaha jamani acheni kunichekesha eti mwisho wa dunia 2012,wangapi walisema ingekua 2000 watu wakaacha hadi shule mbona haikutokea?acheni kujidanganya jamani.mwisho wa dunia ni siku yako ya kufa.hata kesho waweza kua mwisho wa dunia kwako.hahhahahhahha.

  13. Anonymous says:

    haiingii akilini mtu amepewa ada hela ya matumizi imetoka sawa ka wote afu mtu ale ada, agonge yai na kula bia wakati wengine wanajibana afu aseme achangiwe au aombewe ili asilipe. huo ni wendawazimu na kila mdaiwa lazima alipe anachodaiwa. chuo sii cha mjombaako wala elimu si bwerere

  14. Anonymous says:

    we ni shoga huwezi kumuombea mtu asilipe unajua unachoongea? imekula ada ngoja wakione cha moto

  15. Anonymous says:

    HATULIPI NA HATUFUKUZWI.TUMEKUJA WOTE HAPA? KAMA NI KULITIA HASARA TAIFA MBONA MAFISADI WANAIBA MIHELA KIBAO NA NDUGU ZAKO WANAKUFA NJAA HUSHANGILII AU HUJUI HILO

Post a Comment