Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - WANAFUNZI SITA CHUO KIKUU LUMUMBA WAITWA NYUMBANI. MMOJA KATI YAO AMEJIUNGA CHUONI 2008. MKATABA WAVUNJWA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter jumatatu 8/12/2008 saa 14:30 THE THOMCOM Imepata habari zisizo rasmi kuwa kuna wanafunzi sita toka chuo kikuu cha urafiki Lumumba Moscow Russia wameitwa nyumbani kwa kosa la kuvuruga amani. Inasemekana kuwa pindi watakapofika nyumbani watakabiliwa na mkono wa sheria. Inasemekana kuwa waraka wa kuwarudisha nyumbani wanafunzi hao umesainiwa na Mh. naibu waziri na kuwasilishwa chuoni kupitia ubalozi wa Tanzania. Wanafunzi hao ambao majina yao hayakupatikana mapema kutokana na chanzo cha habari hii, watapewa taarifa za kuondoka kwao leo jumatatu saa kumi kamili na Msaidizi wa Rector wa International Relation. Taarifa nyingine zisizo rasmi, INASADIKIKA kwamba mkataba uliosainiwa kati ya Tanzania na Chuo cha lumumba mwaka 2005 na kuhakikiwa mwaka 2007 umevunjwa. Kutokana na Ofisa mmoja chuoni Lumumba, wanafunzi hao wameivamia ofisi moja chuoni hapo, na kuwatolea maafisa maneno makali na ya kutisha. Haikufahamika mara moja ni wanafunzi gani wamefika ofisini hapo leo asubuhi na ni hatua gani zitakazochukuliwa na chuo katika swala hilo. Kati ya wanafunzi hao sita, inasemekana mmoja kati yao ni mwanafunzi aliyejiunga na chuo kikuu cha urafiki Lumumba mwaka 2008/2009 ambapo amedumu chuoni kwa muda wa takribani mwezi mmoja na kwa kawaida, hata hajapata usajili au residence permit na huenda hata hajaanza masomo ya awali ya Lugha. THE THOMCOM inaahidi kufuatilia sakata hili kwa ukaribu na kuwaletea mfululizo mzima wa sakata hili kwa usahihi zaidi na uhakika.
MOSCOW 2008
Tags:

0 comments

Post a Comment