Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Waislamu wasisitiza Tanzania ijiunge OIC Na Salim Said

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MAELFU ya Waislaam nchini wameitaka serikali itekeleza hatua za Tanzania kujiunga na Jumuiya Nchi za Kiislaam (OIC) kwa manufaa ya watu wake. Waislaam hao ambao wamekusanyika katika Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam jana walimesema kwa kuwa serikali imefanya uchunguzi na kujiridhisha kwamba OIC haina madhara kwa taifa isipokuwa manufaa ya kiuchumi basi inatakiwa kujiunga. Akiwasilisha tamko la Waislaam kuhusiana na hoja ya OIC, Msemaji Mkuu wa mhadhara huo ulioandaliwa na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Mwinyikai Mzee aliitaka serikali ijiunge na OIC kwa manufaa ya Watanzania wote. “Kwa kuwa serikali imefanya uchunguzi na kujiridhisha kwamba OIC haina madhara kwa taifa isipokuwa manufaa ya kiuchumi, tunaiomba ijiunga na OIC mara moja,” alisema Mzee. Alisema wanachotarajia ni kwamba serikali iliyopo madarakani itekeleze ahadi zake kwa wapiga kura ambazo ilizitoa ilipokuwa ikijinadi katika kampeni za uchaguzi 2005. Alifafanua kwamba wanatumai kuwa pande zote zinazohusika zitatumia busara katika kutekeleza ahadi hizo kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu. Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Msikiti wa Idrissa, Sheikh Ally Basaleh alisema OIC inatafsiriwa vibaya ambapo tafsiri sahihi ni Kongamano la Jumuiya za Kiislaam na si Jumuiya ya Nchi za Kiislaam. “Hii ‘C’ ni ‘conference’ na si ‘country’ kama inavyotafsiriwa na watu mbalimbali pamoja na vyombo vya habari,” alisahihisha Basaleh. Alifafanua kwamba katika utendaji wa OIC nchi ndio inaulizwa kuhusu kitu gani cha kufanyiwa na wala haulizwi mtu mmoja au dini fulani. Alisema, kama serikali itasema ijengewe daraja la Kigamboni watakaofaidika ni wananchi wote waislaam na wakristo. “Kama serikali itasema ijengewe daraja la Kigamboni watakaofaidika ni wananchi wote waislaam na wakristo,” alisema Sheikh Basaleh. Tamko hilo lilisainiwa kwa ridhaa ya Waislaam wote nchini na makatibu wakuu wa taasisi sita za kiislaamu zilizopo Tanzania.
Tags:

0 comments

Post a Comment