Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kashfa ya kutumia vibaya madaraka kwenye IMF

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Kashfa ya kutumia vibaya madaraka kwenye IMF

New York

Fuko la fedha la kimataifa la IMF limeanza uchunguzi juu ya mkurugenzi wake kwamba alitumia vibaya madaraka yake. Uchunguzi unafanywa ili kutafuta uhusiano Dominique Strauss-Kahn aliyekuwa nao mapema mwaka huu na afisa aliyekuwa chini ya mamlaka yake na ambae aliondoka ofisini.

Kulingana na gazeti la soko la hisa la mjini New York nchini Marekani la Wall Street, kashfa hiyo inamhusisha afisa mkuu katika kitengo cha Afrika cha IMF. Dominique Strauss-Kahn, waziri wa zamani wa fedha wa Ufaransa, amesema amekuwa akishirikiana na mawakili waliokodishwa na IMF kufanya uchunguzi. Uchunguzi huo wa IMF unafanyika mwaka moja baada ya rais wa zamani wa Benki ya dunia, Paul Wolfowitz, kulazimika kujiuzulu kufuatia makelele ya wafanyakazi juu ya hatua yake ya kuruhusu malipo ya kupita kisiasi kwa rafiki yake ambae alikuwa akifanya kazi katika benki hiyo.

Tags:

0 comments

Post a Comment