|
Kura za maoni zinaonyesha kuwa Barack Obama ameongoza tangu kuanza kwa mwezi Oktoba. |
Katika jimbo moja linaloweza kunyakuliwa na mgombea yoyote, North Carolina, mwamko wa upigaji kura za mapema kwa upande wa wafuasi wa chama cha Democratic umepanda kwa asilimia 400 katika wiki ya kwanza ya shughuli hiyo, kama ilivyo kwa majibo ya Ohio, Iowa, Nevada na New Mexico.
Kazi ya kura za mapema sasa inaendelea katika majimbo 34, ingawa siku rasmi ya uchaguzi ni Novemba 4.
Takriban theluthi moja ya wapiga kura wanatarajiwa kufanya kazi hiyo kabla ya Novemba 4, ikilinganishwa na mwaka 2004.Miaka ya nyuma, chama cha Republican kilionekana kunufauka zaidi kwa mfumo huo.
"Hii ni taswira-akisi ya yale tuliyokuwa tukiyashuhudia miaka ya nyuma," anaeleza Paul Gronke wa kituo cha maelezo ya upigaji kura wa mapema[Early Voting Information Center] kwenye chuo cha Reed. "Hizi haziwezi kuwa habari njema kwa John McCain".
Kwa ujumla, upigaji kura za mapema unafanyika katika majimbo mengi zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2004.
Kwenye majimbo ambayo husajili wapiga kura kulingana na vyama vyao, uhusiano wa vyama na wapiga kura wa awali unajulikana - ingawa hakuna uhakika endapo wanachama wote wa Democratic waliojiandikisha watampigia kura mgombea wao na takwimu hazionyeshi jinsi watu wasioegemea upande wowote wanapiga kura vipi.
Takwimu Mojawapo ya sababu za kutumika kwa upigaji kura wa mapema ni kutoa fursa kwa watu wanaojaribu kuepuka misururu mirefu kusubiri kupiga kura siku ya uchaguzi - ambayo kuna uwezekano tatizo likaongezeka mwaka huu kutokana na idadi kubwa ya wapiga kura.
John McCain anajaribu kumpiku Barack Obama katika muda uliosalia. |
Kwenye wilaya ya Clark, jimbo la Nevada, ambayo inajumuisha jiji kubwa zaidi la Las Vegas, wafuasi wa chama cha Democratic wamewazidi kwa idadi wale kwa uwiano wa moja kwa mbili, ongezeko la asilimia 52 juu ya kura alizopata John Kerry, mgombea wa chama cha Democratic kwenye uchaguzi wa mwaka 2004.
Eneo la Cuyahoga huko jimbo la Ohio, ambalo linajumuisha jiji la Cleveland, kumekuwa na wapiga kura wa mapema 45,000 wa chama cha Democratic na chama cha Republican kimepata 10,000 Republican, idadi kubwa kuliko aliyoipata John Kerry katika uchaguzi wa mwaka 2004.
Kwenye jimbo la New Mexico, ambalo George W Bush alishinda kwa kura 6,000 mwaka 2004, wanachama wa Democratic wamejitokeza mara mbili zaidi kupiga kura za mapema.
Na huko North Carolina, jimbo ambalo limekuwa mikononi mwa Republican lakini sasa halina mwenyewe, kati ya watu 480,000 waliopiga kura za mapema, asilimia 54 ni wafuasi wa chama cha Democratic, wakati asilimia 27 ni wa Republican, na asilimia 16 ni watu wasioegemea upande wowote.
0 comments