Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - ETI SEMENI WADAU...

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter HIVI INAWEZEKANAJE WATU KUKANYAGANA KATIKA UKUMBI WA STAREHE (DISCO) KIASI CHA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 19? KWA KAWAIDA WATU HUKANYAGANA PALE AMBAPO IMETOKEA AJALI AMBAPO HUWA KILA MTU ANATAFUTA NJIA YA KUJIOKOA. TUKIO LILILOTOKEA TABORA HIVI KARIBUNI LINATIA WASI WASI SANA KWA WATOTO 19 KUFARIKI ETI KWA KUKANYAGANA KATIKA UKUMBI WA DISCO WAKATI WA SHEREHE ZA IDD BILA MAELEZO ZAIDI. TUACHE KUDANGANYANA BWANA! UCHUNGUZI UFANYIKE HARAKA NA UKWELI UWEKWE HADHARANI..... ETI SIKIA HIYO NDIO RIPOTI...... Polisi katikati ya Tanzania imesema takriban watoto 19 wamekufa baada ya kutokea mkanyagano kwenye ukumbi wa Disco wakati wa sikukuu ya Idd.

Tukio hilo la kukanyagana ndani ya ukumbi wa disco limetokea katika mkoa wa Tabora kilometa 750 kaskazini magharibi mwa mji wa Dar es Salaam.

Disco hilo hilo lilikuwa limeandaliwa kama sehemu ya sherehe za Idd al-Fitr kuadhimisha kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waliokufa katika mkasa huo ni vijana kati ya umri wa miaka 12 na 17.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora Daudi Siasi, ameliambia Shirika la Utangazaji la Tanzania, kwa mujibu wa uchunguzi wa awali vijana hao 19 walikufa kutokana na kukanyagana na wengine kukosa hewa wakiwa ndani ya ukumbi wa disco.

Kamanda Siasi amesema watu kadha walitibiwa hospitalini kutokana na majeraha waliyopata.

Uchunguzi wa polisi bado unaendelea.

Tags:

0 comments

Post a Comment