Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - EPA: Wamiliki wa KAGODA Agriculture ltd watajwa kwa majina

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Mwanaharakati mmoja amejitokeza na kuwataja kwa majina wamiliki wa Kagoda Agriculture ltd ambao walikuwa hawafamiki. Mwanaharakati huyo akionesha nyaraka za ushahidi wa makaratasi, na kudai kuwa na ushahidi wa Audio na video amesema ameshawasilisha ushaidi huo kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili wamiliki hao waweze kufikishwa mahakamani.
Majina yaliyotajwa ni kama ifuatavyo: wa kwanza na kinara wa Kagoda ni Rostam Aziz, wa pili ni Yusuf Manji, Braham Abdulasundi Chakari, James Kato, Bahati Goda na mwanamama Thabu Mwasura Omari. Mwanaharakati huyo alisema sio kweli kama ilivyokuwa imebainika hapo awali kuwa wamiliki wa Kagoda ni John Jowendo na Fransis Willium bali waliosaini makaratasi ni James Kato na Bahati Goda ambao majina yao ukiunganisha unapata neno KAGODA kwa maelekezo ya Rostam Aziz.
Manji anahusika kwa kudhamini kufungua account namba 01J1021795700 katika bank ya CRDB Tawi la Holland kiasi cha dola milion 2 na kutoroshwa kwenda Dubai kwa Mafungu mafungu. Hadi kufikua tarehe 31/3/2006 Account hiyo ilikuwa tayari ina dola 9 084 762,64.
Ameendelea kusema kuwa baada ya serikali kutaka fedha hizo zirudishwe, kiasi fulani cha fedha kilirudishwa na zilizobaki ziliendelea kumilikiwa na wajomba wa Rostam Aziz.

0 comments

Post a Comment