Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Waziri afuatwa na mkewe bungeni

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Dodoma
Mke wa Waziri wa Serikali ya Tanzania anayetumikia wizara nyeti, (jina limehifadhiwa), amemuibukia mumewe bungeni kisa uwepo wa muigizaji Wema Abraham Sepetu aliyekuwa mjini hapa hivi karibuni.


Tukio hilo lilijiri ndani ya Viwanja vya Bunge mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mwanamama huyo alionekana akizama maeneo hayo na ‘kumtaiti’ waziri huyo ambaye hupendelea kujiachia kwenye kumbi za starehe.


‘Shushushu’ wa Ijumaa alifanikiwa kunusa ‘infomesheni’ kwamba ‘wife’ huyo alipopata habari kuwa timu ya wasanii wanaozitengeneza fedha kupitia Bongo Movie itakuwa mjini hapa kukipiga na wabunge, naye alifunga safari kutoka Dar es Salaam kumfuata mumewe kwa kuwa anamfahamu vilivyo hasa linapokuja suala la ‘totoz’ zenye majina.


Hata hivyo, mwanamama huyo ambaye alitia maguu kwenye mechi ya waheshimiwa na wasanii hao, alipokutana na wabunge wanawake wanaofahamiana alisikika akisema kuwa ameibuka kulinda ‘mali’ zake kwa kuwahofia mastaa wa kike wa filamu huku jina la Wema likitajwa mara tisa.


“Mhh! Mama (jina la waziri) naona umekuja kulinda vyako au unaogopa waigizaji watakuzidi?” Alisikika mmoja wa waheshimiwa hao.


Mwishoni mwa wiki iliyopita, timu hizo zilikipiga mjini hapa ambapo waheshimiwa wabunge waliwanyamazisha waigizaji ambapo wanaume walipigwa 2-1 huku wanawake wakitandikwa 17-11.

0 comments

Post a Comment