Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Redio Sweet FM yateketea

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KITUO cha redio cha Sweet Fm kilichopo jijini Mbeya, kimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana na kusababisha hasara kubwa.

Mkurugenzi wa kituo hicho Joseph Mbuza akizungumza na waandishi wa habari jana alisema ajali hiyo ya moto imetokea usiku wa kuamkia jana, na kuunguza studio ya redio hiyo na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Alisema mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini inahisiwa kuwa ni hitilafu ya umeme, huku thamani halisi ya mali zilizoteketea katika studio hizo ikiwa bado haijatambulika.

Wakizungumzia ajali hiyo baadhi ya wadau wa habari walisema ni pigo kutokana na mchango wa vyombo vya habari katika mikakati mbalimbali ya maendeleo ya jamii.

Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya, Christopher Nyenyembe alisema kumekuwa na matukio mengi ya ajali za moto katika nyumba na ofisi mbalimbali zinazosababishwa na hitilafu ya umeme.

Alisema ajali hizo zimekuwa zikisababisha hasara huku Tanesco ambayo inawajibika na usambazaji umeme ikishindwa kuwalipa fidia waathirika kutokana na kutokuwepo kwa mikataba na wateja wao.

“Kuungua moto studio hiyo ni pigo katika tasnia ya habari, ingawa bado uchunguzi unaendelea kuhusu chanzo cha tukio hilo lakini uchunguzi wa awali unaonesha ni umeme.

“Wakati umefika kwa Tanesco kuwa na mikataba ya wazi na wateja wake kwa lengo la kuwafidia hasara wanapopata majanga kama haya,” alisema Nyenyembe.

0 comments

Post a Comment