Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Zitto aitaka Tanesco iache kuzalisha umeme

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma, imelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuyaachia mashirika ya umma jukumu la kuzalisha umeme na kujikita zaidi katika shughuli ya kujenga na kusimamia miundombinu ya kusafirishia nishati hiyo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kabwe Zitto, ameyasema hayo Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari, katika semina ya wiki moja inayoendelea ya wabunge.

Zitto alisema, ni vyema bajeti ya shirika hilo ikaegemea zaidi kuimarisha miundombinu hiyo ambayo kwa sasa ni chakavu na haina uwezo wa kutosha badala ya kuendelea kukopa fedha nyingi kwa kuzalishia umeme wakati yapo mashirika ya umma nchini yenye uwezo wa kuzalisha nishati hiyo bila kuwa mzigo kwa Serikali.

“Wakati umefika kwa Tanesco badala ya kuhangaika na kuzalisha umeme, bora wakaacha jukumu hilo lifanywe na mashirika ya umma ambayo yapo nchini, tena yenye uwezo wa kuifanya kazi hiyo,” amesema Zitto.

Amesema, iwapo mashirika ya umma yatapewa nafasi zaidi ya kuzalisha umeme kwa uwezo yaliyonayo, baada ya miaka mitano, hali ya umeme nchini itabadilika kutokana na uwezekano mkubwa wa kumaliza wa vyanzo mbalimbali vya kuzalisha umeme vilivyopo nchini kuanza kutumika.

Amevitaja baadhi ya vyanzo hivyo alivyodai ni Tanzania pekee kati ya nchi za Afrika Mashariki inajivunia kuwa navyo lakini bila kuvitumia ipasavyo kuwa ni Liganga, Mchuchuma, Ngaka na Kiwira ambavyo kwa pamoja vina uwezo za kuzalisha megawati 1,500 za nishati ya umeme, inayotosha kumaliza tatizo lililopo la umeme kwa miaka 150 ijayo.

Pia ameitaja nishati ya umeme iliyopo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuwa nayo inatosha kumaliza matatizo ya umeme ambapo hatua pekee iliyobaki ni kwa Serikali kuamua na kuchukua hatua za kuharakisha uzalishaji wake.

“Sisi kama Kamati ya Mashirika ya Umma, katika awamu hii tumeamua kuhakikisha kuwa, mashirika ya umma nayo yanashiriki katika hatua zote za kukuza uchumi na kipaumbele ni nafasi yake katika upande wa umeme ambalo sasa ndio tatizo kubwa lililopo,” alisema mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Akizungumzia uchumi, Zitto, alisema ni vigumu kwa sasa kupima hali halisi ya uchumi kutokana na takwimu zilizopo kuangalia zaidi ukuaji wa mashirika makubwa na maeneo ya kisekta ambayo hayamgusi moja kwa moja mwananchi.
Tags:

0 comments

Post a Comment