Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kaburi la Nelson Mandela ladoda

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Baba wa Afrika, Nelson Rolihlahla Mandela, 92 bado yupo hai na mchoro wa kaburi pamoja na eneo aliloandaliwa kuzikwa vimedoda.

Mandela ambaye ni Mwafrika anayeheshimiwa zaidi duniani, aliibua mshtuko mkubwa mwaka uliopita alipozushiwa vifo mara kadhaa pamoja na kuandaliwa maziko yenye hadhi kubwa.

Habari zinasema kuwa kila kilichoandaliwa kwa ajili ya maziko ya Mandela kimedoda, huku kwa baadhi ya watu wakiambulia hasara kubwa.

Mtandao mmoja wa intaneti nchini Afrika Kusini uliandika kuwa waliozikarabati nyumba zao kwa ajili ya kuwapangisha wageni ambao wangehudhuria mazishi ya Mandela wamekubali hasara.

“Harakati za kwenda kijijini hazipo tena. Kuna waliohama makazi yao na kuyakarabati ili wawapangishe wageni nao wamepata hasara, wamerudi kwenye nyumba zao na sasa ni hasara kwao,” alisema Jundini Zehlesa aliyekaririwa na mtandao.

HALI YA KIJIJI CHA QUNU
Habari zinasema kuwa Kijiji cha Qunu kilichopo Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini ni tulivu na aliyepewa ‘tenda’ ya ujenzi wa kaburi hajulikani alipo.

Iliandikwa mtandaoni kuwa mtu aliyepewa jukumu la kujenga kaburi la kifahari na jeneza lenye hadhi ya dunia hajulikani alipo kwa sababu familia ya Mandela inaamini mtu huyo ana siri kubwa.

Ripoti zinasema kwamba kuna ndugu wa Mandela walifikia hatua ya kuuza hakilimiliki ya matangazo ya kifo cha Mandela kwa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) bila kuwashirikisha wengine.

MJUKUU WA MANDELA ACHOTA BIL. 124
Habari zinasema kuwa mvutano mkubwa ulifuatia kubainika kwamba mjukuu wa Mandela ambaye ni Mbunge wa Qunu, Mandla Mandela alichota karibu shilingi bilioni 124 (pauni za Uingereza milioni 54) kutoka SABC.

UVUMI KILA SIKU
Imeelezwa kuwa moja ya vitu ambavyo vimewaweka roho juu wananchi wa Afrika Kusini ni mtindo wa watu kutuma SMS za kutunga wakitangaza kwamba mzee Mandela amefariki dunia.
Tags:

0 comments

Post a Comment