Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Dk Bilal awapasha CUF

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Mgombea mwenza wa mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, amewataka  wananchi wa Wilaya ya Mafia, kuwa makini dhidi ya viongozi wa CUF kwa kuwa chama hicho kimejaa viongozi waongo na wasiotaka Tanzania ipate maendeleo.

Kauli hii ya Dk Bilal inakuja siku kadhaa  baada ya mgombea Urais kupitia tiketi ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, kufanya mikutano yake ya kampeni kisiwani hapa na kudai kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege, gati na barabara ni geresha tu ya CCM na kwamba wananchi wawachague wao kwa kuwa ndio wanaofahamu umuhimu wa maendeleo.

Akizungumza katika kikao cha  wazee wa mji wa Mafia, Dk Bilal alisema  CUF hawastahili kukabidhiwa dola kwa kuwa hawana uwezo na hata pale walipokabidhiwa nafasi hawakuitumia vema zaidi ya kuwaumiza wananchi wanaoishi katika kata wanazoongoza zikiwemo za Mafia.

Mapema, mgombea mwenza huyo alikabidhiwa ripoti kuhusu uongozi wa Kata ya Jibondo inayoongozwa na CUF, na ripoti hiyo ilisema miradi mbalimbali ya maendeleo imesimama  yakiwa ni matokeo ya misimamo ya uongozi wa CUF.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule na ile ya maji hali, inayowafanya wananchi kubaki nyuma kimaendeleo.

Akizungumza baada ya kupewa nafasi, mgombea ubunge wa jimbo la Mafia kupitia CCM, Abudkadir Shah, alisema, wakati wa uongozi wake, jimbo hilo alifanikiwa kujenga shule za sekondari za kata katika kata zote za CCM .

Alisema pia alijitahidi kuzipatia huduma za maji lakini kila alipojitahidi kutoa huduma hizo katika kata zilizoko chini ya CUF, aligonga mwamba.

Akizungumza na wananchi wa Mafia, Dk. Bilal ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Pwani, alisema wananchi na wapenzi wa CCM wanatakiwa kujifunza hasa kwa watu wa Unguja, juu ya  tabia zisizo za kidemokrasia ambazo wanachama na viongozi wa CUF wanazo. 

Dk. Bilal pia aliwafahamisha wananchi wa Mafia kuwa, barabara yao kuu inayounganisha pande zote za Kisiwa hicho yenye urefu zaidi ya kilometa 50, ipo katika ilani ya CCM na hatua za kuijenga katika kiwango cha lami zinaendelea.

Katika mkutano mwingine na wazee wa Mafia, Dk. Bilal aliwaambia wazee hao kuwa, CCM ni chama kikongwe ambacho kina historia na mambo mengine mazuri ambayo wengine wanajifunza na wangetamani sana kuona wanaongoza nchi zao kama ilivyo CCM.
Tags:

0 comments

Post a Comment