IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk John Magufuli, amekubali kurudisha katika Kamati ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya miswada miwili kuhusu mifugo.
Hatua hiyo imekuja baada ya wabunge kadhaa, kupinga miswada hiyo kwa madai kuwa ilikuwa inalenga, kuwanyanyasa wafugaji.
Miswada hiyo ni ule wa utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo ya mwaka 2010 na wa sheria ya malisho na vyakula vya mifugo wa mwaka 2010, iliyowasilishwa bungeni jana, lakini baadhi ya wabunge waligoma kuiunga mkono.
"Miswada hii ingepitishwa ingekuwa kitanzi kwa serikali maana isingefanya operesheni ya ajabu. Sheria hiyo ingeibana serikali," alisema Magufuli
Msimamo wa wabunge dhidi ya miswada hiyo iliyokuwa imewasilishwa bungeni na waziri Magufuli, ulianzishwa na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, alipomuomba Naibu Spika wa Bunge, Anna Makinda, atoe mwongozi wa kama anaweza (Ole Sendeka) kuomba miswada hiyo urudishwe na isijadiliwe na Bunge, hadi hapo utakapofanyiwa mabadiliko.
Mbunge huyo alisema kifungu cha 61 na 69 kinatoa mwongozo kuwa mbunge anaweza kuomba hoja inayojadiliwa irejeshe kuandaliwa upya na kujadiliwa tena na Bunge.
Kutokana na hoja hiyo Naibu Spika Anna Makinda aliamua kumuokoa waziri Magufuli, kwa kumtuliza mbunge huyo kuwa kifungu cha 61 kiko wazi na kimtaka mbunge aeleze sababu za ombi.
Alisema hata hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa muswada huo, anatumia kifungu cha 69 kuruhusu majadiliano yaendelee ili serikali ipate mawazo zaidi kuhusu na miswada hiyo.
"Kwa mamlaka niliyonayo nami natumia kifungu cha 61 kifungu kidogo cha 2 kuruhusu mjadala huu uendelee ili serikali ipate mawazo ya wabunge wengine. Mjadala unaendeleoĆ¢€ alisema Makinda
Hata hivyo uamuzi huo ulichochea moto kwa mbunge aliyefuata kukosoa miswada hiyo.
Mbungwe huyo, alikuwa ni George Simbachawene (Kibakwe) ambaye alipinga vikali muswada wa utaifishaji wa mifugo ya wafugaji kwa kisingizio ya kuwa mingi.
"Sheria hii ina lengo la kuwafuta wafugaji, mnaweka sheria ya kusajili mifugo yao wakati tumeshindwa kusajili magari, nenda Dar magari yamerundikana watu wameshindwa kusajili, kabla ya kusajili mifungo hebu tuanze kwanza na magari haya tuondokane na msongamano barabarani," alisema.
Kwa upande wake, Mbunge wa Longido (CCM) Michael Lekure, alipinga kuunga mkono muswada huo kwa maelezo kuwa hauzingatii utawala bora
"Nilitegemea muswada huu utazingatia utawala bora, na ungewasaidia wafugaji lakini badala yake, umeonyesha kuwa ni wa kuwanyanyasa," alisema.
"Kwa sababu moja au nyingine siuungi mkono muswada huu," alisisitiza mbunge huyo.
Lazier alisema kwa yeye kuunga mkono miswada hiyo ni sawa na kuwasaliti wafugaji ambao walimpigia kura pamoja na Chama Cha Mapinduzi, ili awawakilishe katika Bunge.
Aliungana na Ole Sendeka kutaka muswada huo urudishwe na kuandaliwa upya kabla ya kuwasilisha tena bunge kwa majadiliano.
Mbunge wa Kiteto (CCM) Benedict Ole Nangolo, alisema muswada ni nakala ya utafiti wa mwanafunzi wa shahada ya falsafa ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Texas nchini Marekani.
You Are Here: Home - - Magufuli 'asalimu amri' kwa wabunge
0 comments