MOSCOW
Urusi imesema kuwa mtambo wake nyuklia iliyoujenga nchini Iran uko tayari kuanza kufanya kazi. Waziri Mkuu wa Urusi, Vladmir Putin, amesema mtambo huo uliyojengwa katika mji wa Bushehr utakuwa tayari kufanyakazi katika kipindi cha majira ya joto.
Waziri wa Mambao ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameitetea hatua hiyo akisema kuwa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki limekuwa likiichunguza Iran kuhakikisha kuwa inatimiza masharti yake ya kuzuia utapakaaji wa silaha za silaha za nyuklia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, haraka ameulaumu uamuzi huo, akisema kuwa umechukuliwa mapema mno, hasa ikitiliwa maanani bado hakuna uhakika wa azma ya Iran katika mpango wa nyuklia.
Marekani inaongoza jitihada za kutaka Umoja wa Mataifa uiwekee duru ya nne ya vikwazo Iran, katika harakati za kuizuia nchi hiyo kuendelea na mpango wake huo wa nyuklia.
0 comments