Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wanajeshi wadaiwa kuua mtoto wa Chifu Fundikira

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani Mhe. Amani Abeid Karume, Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Ali Mohamaed Shein (kushoto) Rais Mstaafu Mzee Ali Hassani Mwinyi (kulia), na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Saleh Ramadhani Feruzi wa pili (kulia) wakikiingia katika ukumbi wa mkutano tayari kuanza kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar jana.

RAIS wa Zanzibar na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM visiwani, Aman Abeid Karume ameyawasilisha rasmi maridhiano aliyofikia yeye na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambapo kimsingi suala la serikali ya mseto limekubaliwa.

Rais Karume aliyasema hayo kwenye kikao kilichofanyika jana kuanzia saa nane mchana hadi saa moja usiku kikiwa chini uenyekiti wake na kuhudhuriwa na miongoni mwao, Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

Zanzibar imekuwa na matumaini ya kumalizika kwa siasa za chuki tangu Rais Karume afanye mazungumzo na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Novemba 5, mazungumzo ambayo yalisababisha chama hicho kitangaze kumtambua Karume kuwa rais wa visiwa hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zbar, Saleh Ramadhani Feruzi alisema Rais Karume alikifahamisha kikao hicho kilichokuwa na ajenda kuu tatu, kuhusiana na mazungumzo yake na Maalim Seif akisema kuwa mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kuijenga Zanzibar mpya.

Maridhiano hayo yaliyosababisha hoja binafsi ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, yameishtua CCM ambayo ililazimika kukutana mara kwa mara ikiwamo mkutano wake uliofanyika Zanzibar jana.

Alhamisi wiki hii kiongozi wa kambi ya upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari aliwasilisha hoja binafsi kutaka kutenguliwa kwa vifungu vya Katiba ya Zanzibar ili kuweka mazingira ya Zanzibar kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa.

Akieleza kiurefu kidogo Feruzi alisema kikao hicho kimeelezwa kuwa maridhiano hayo lengo lilikuwa kusamehena, kujenga Zanzibar mpya yenye maelewano na kuendesha siasa za kistaarabu za kupingana bila kupigana.

Alisema kuwa ajenda ya pili katika kikao hicho ilikuwa ni kuhusiana na tetesi za mitaani zinazokuzwa na vyombo vya habari na kuchangiwa na wanasiasa ya kuwa Rais Karume anataka kuongeza muda wa urais atakapomaliza kipindi chake cha uongo mmoja.

Lakini alisema kuwa kikao hicho kilipokea taarifa kwamba Rais Karume alisisitiza misimamo wake alioutoa Januari 12, mwaka huu katika uwanja wa Gombani Pemba kwamba kipindi chake cha kuwapo madarakani kimekwisha kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na hawezi kuendelea.

"Yeye mwenyewe amesema hatooongeza hata siku moja ya kuwapo madarakani,"alisema Feruzi.

Kuhusu ajenda ya tatu alisema ilihusiana na hoja binafsi inayotaka kuwasilishwa katika baraza la wawakilishi na kiongozi wa kambi ya Upinzani Abubakar Hamis Bakari kuhusiana na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Katika hoja hiyo alisema kuwa wajumbe walitaka hoja ya maazimio yaliyofikiwa Butiama yazingatiwe yaliyotaka suala la muafaka lisubiri maoni ya wananchi wa Zanzibar kabla ya kuchukua hatua yoyote ile.

Alisema kuwa kimsingi wajumbe walitaka kujiridhisha juu ya azimio hilo kwa kuwa wengi wao walishasahau waliazimia nini katika kikao cha Butiama 2008 kwa hiyo ikabidi lisomwe upya.

Baada ya kulisoma likajadiliwa baada ya kujadiliwa wajumbe wote walikubaliana kwamba hoja binafsi ipelekwe Baraza la Wawakilishi na wajumbe watajua namna ya kulijadili na kulipitisha.

Lakini katika Chama cha CCM wajume wote walitoka na msimamo mmoja kwamba wanaunga mkono azimio la Butiama na waliona halina matatizo yoyote na wameunga mkono suala la kuwapo serikali ya umoja wa kitaifa.

Hata hivyo kabla ya kikao hicho Rais Karume alikuwa kikao tangu saa tatu asubuhi hadi saa saba na nusu mchana na wenyeviti wote wa mikoa. Jana Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha alifanya kikao asubuhi na baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi.
Tags:

0 comments

Post a Comment