IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Dr. Slaa
tunashukuru kwa ufafanuzi wako makini.
SWALI: Katika ufuatiliaji wako wa lile sakata la CCM kuingiza magari
na kukwepa kiasi kikubwa cha kodi, je walikwepa kiasi gani? na je,
wamelipa kiasi walichokwepa?
..............................................................................................
JIBU: Kwanza naomba niwasalimie wote na kuwashukuruni sana kwa dhati kwa
maswali mengi ambayo yameendela kuja pamoja na kuwa majibu yamechukua
muda mrefu. Kutoa tarehe 12 Januari, nimekuwa na Kamati ndogo ya
Kamati ya LAAC ambaye ilifanya ukaguzi wa mahesabu ya Halmashauri za
Wilaya ya Bagamoyo (Pwani), Halmashauri ya Korogwe Vijijini (Tanga),
Muheza (Tanga), Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha na Halmashauri ya
wilaya ya Simanjiro. Ukaguzi huo umeendana na kukagua miradi
mbalimbali (site inspection-Value for Money Audit. Hivyo mnavyoona
ilikuwa vigumu sana kuingia kwenye mtandao kwa kipindi chote hicho.
Kutokana na uwingi wa maswali, nitajaribu kuyaweka yale yote
yanayofanana katika kundi mmoja, na mengine nitayajibu kwa mtiririko
jinsi yalivyokuja. Iwapo kwa mtindo huu mtu hataridhika, bado anaweza
kuomba afafanuliwe kwa kina zaidi, pale na nitafanya hivyo pale
inapowezekana.
Pili, hakuna haja ya kutukanana ndugu zangu. Tulikubaliana kuwa na
mtandao ambao wote tunaheshimiana, tunaelimishina pale ambapo mtu
haelewi, na hata yule mwenye ajenda yake hakuna haja ya kumtukana.
Uvumilivu ni jambo kubwa sana katika mtandao kama huu unaojumuisha
watu wa itikadi mbalimbali, imani mbalimbali, falsafa zinazotofautiana
na pengine hata tamaduni zinazotofautiana. Iwapo mtu anaona ametukanwa
badala ya ku react, ni vema aka "Ignore"( puuza) hakuna kinachouma
kama kumpuuza mtu kama ni mwelewa.
i) Wachangiaji kadhaa, akiwemo Mzitto Kabwella, Omarilyas, na wengine
wamependa nitoe ufafanuzi zaidi kuhusu
a) Swala la Zitto kumpinga Katibu Mkuu wake hadharani. Niseme tu, kuwa
swala hili nilikwisha kulitolea ufafanuzi, sidhani kama lina haja ya
kuliendeleza zaidi. Zitto kwa sasa hivi yuko Ujerumani akimalizia
masomo yake. Mara kadhaa amekuwa akifika Dar na kila mara amkuwa
akiwasiliana nami, na kunipa picha ya majadiliano yanayoendelea kwenye
vyombo vya Habari. Nadhani itoshe kusema tu kuwa sioni umuhimu wa
kuendeleza swala hili kwani kinachoonekana migogoro wakati mwingine
imepandikizwa kwa malengo, wakati mwingine inaweza kuwa na dalili za
ndani lakini nilikwisha kulitolea maelekezo na ngazi za chama nazo
zilikwisha kulitolea maamuzi. Nadhani muhmu zaidi ni kujenga utamaduni
wa kuvumiliana pale ambapo kauli zinaweza kutofautiana, na hazina
madhara kwa chama, mathalan chama kinachoamini katika misingi sahihi
ya demokrasia ya kweli. Kama nilivyosema, Tafsiri ndani ya chama
isitafsiriwe kwa mtu mmoja au wawili, bali kama ni vikundi ni lazima
kuwe na utafiti wa kina kujua vikundi hivyo vinaathiri chama kiasi
gani, viko vingi au vina wafuasi wengi kiasi gani, na kama vikundi
hivyo havikutengenezwa mezani kama ilivyotokea wakati wa Kafulila
ambapo ilitengenezwa mezani kuwa kuna wenye viti 11 wa Mkoa wanamwunga
mkono Kafulila. Ukiwauliza wawataje, na hata Gazeti liliwachapisha
linaposhindwa kuwathibitisha basi ni dhahiri kuna msingi wa umbeya,
majungu na uchochozi wenye ajenda iliyojificha.
b) Mgogoro katika chama cha siasa unapimwa kwa vigezo muhimu kama vile
je, vyombo vya maamuzi, Kamati Kuu, Baraza Kuu, Mkutano Mkuu
vimegawanyika kwa kiwango gani. Iwapo vyombo vya maamuzi viko united,
mtu mmoja mmoja anayetofautiana na kauli ya wengi ni dhahiri hawezi
kuwa tishio na akishikilia msimamo wake hawezi dhahiri pia kuwa mwana
demokrasia. Vigezo hivyo hivyo, ningelipenda tuvitumie pia kuipima
CCM, hasa kwa wale wanaopenda nitoe kauli yangu kuhusu vikundi na
mgogoro ndani ya CCM. Vigezo vyovyote vya kisayansi ni lazima kwanza
vita "Establish" criteria/parameters zinazoweza kuwa proved
"empirically". Vinginevyo inaweza kubaki kuwa propaganda. Hii haina
maana ya kusema kuwa tahadhari na hatua ya kuziba ufa zisichukuliwe
mapema. Lakini uchukuaji wa hatua hizi ni pamoja na kupima faida na
hasara ya hatua hizo.
c) Swala la Zitto kumsaidia Kafulila nalo nilikwisha kulifunga. Iwapo
Vyombo vya maamuzi vitaona kuwa hatua hiyo inavunja Katiba, Kanuni na
Maadili ya Chadema, hatua stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa Katiba
na Taratibu za ndani ya Chadema. Huu ndio utaratibu sio kwa Zitto tu
lakini kwa viongozi wote wa ngazi ya Kurugenzi ambao mamlaka yao ya
Nidhamu ni vyombo vya Juu yaani Kamati Kuu/Baraza Kuu au Mkutano Mkuu
kadiri itakavyokuwa.
d)Swala la Kufulila kuitwa "Sisimizi" kama alivyouliza Magezi nadhani,
tukubali kuwa kuna lugha ya kuongea na lugha ya kuandika, na hasa
inapotumika "analogy". Neno Sisimizi katika analogy hii ilionyesha
level ya Kafulila inaishia wapi, kwa vile kama ilivyoripoti yeye
mwenyewe na baadhi ya vyombo vya habari vikataka kujenga dhana kuwa
mamlaka yake ya nidhamu ni au Kamati Kuu au hata juu ya hapo.
Nashukuru kuwa neno sisimizi lilieleweka haraka na watanzania na wale
wote wanaojua ngazi za mamlaka. Kauli zinapaswa kuchukuliwa ndani ya
"context" iliyotumika kupata maana halisi ya kinachomaanishwa na
msemaji.
e) Mzitto pia ameliongelea swala la ukabila ndani ya Chadema. Sina
uhakika Mzitto ana background gani, na kwa bahati mbaya hatumii jina
lake halisi. Sidhani kama kuna mwandishi yeyote makini, au mwanasiasa
ambaye kweli ni mwanasiasa anaamini kuna ukabila ndani ya Chadema,
hasa kwa maana inayojengwa sana, ya Uchagga. Nimelitolea ufafanuzi
mara kadhaa swala hili, Tumetoa mpaka majina ya viongozi wakuu wa
Chadema, Wakurugenzi wa Idara za Makao Makuu na Kamati Kuu.
Tumeonyesha kabila la kila mhusika, mahali anapotoka. Wale wote wenye
nia njema wameelewa, lakini ambao kwa makusudi "hawataki kuelewa" kwa
sababu zao za kisiasa ni kipropaganda hatuna namna ya kuwasaidia. La
muhimu umma mkubwa wa Tanzania umeisha kuelewa chadema hakina ukabila,
wala udini. Kwa mara nyingine, ninatoa challenge, kwa yeyote wenye
ushahidi wa ukabila Chadema auweke hadharani kwenye mtandao huu, ndiyo
namna pekee ya kuondoa majungu na umbeya. Vinginevyo hatuwezi kuimba
wimbo huo huo kila siku, hasa tunapojua ni uwongo wa wazi.
Ni imani yangu nimeweka wazi bila kuficha jambo lolote. Mtu asipotaka
kuamini sasa hapo ni hiari yake, kwani waswahili husema, punda unaweza
kumpeleka mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.Nawashukuru
sana
Mfwatiliaji,
i) Kama nilivyosema, kiasi kilichokwepwa ni zaidi 6 Billion. Wameanza
kulipa sijapata taarifa ya mwisho kama wamemaliza kulipa zote.
2) Jambo baya zaidi, wakati ninazungumzia taarifa ya ccm kuagiza
magari 200 hatukujua kuwa wanaleta Bungeni mswada wa sheria ambao
unapiga marufuki uagizaji wa Magari, nyenzo, vifaa vya uenezi
( bendera, kadi) na au uingizaji wa Helcopter. Sasa ndio tumejua
kwanini waliagiza mapema hivyo, na kuna taratibu nyingine tunafuatilia
ambazo nazo zimefanywa kwa hila hivyo hivyo. Tatizo ni kuwa wenzetu
wanapewa Taarifa muhimu na Serikali, na hivyo kufanya uwanja wa Siasa
usiwe Level play ground, kama tulivyodai siku zote.
3) Tunafuatilia hata fedha zilizotumika, watu waliotumika kuagiza
magari hayo wako safi kiasi gani au ni EPA nyingine. Ndiyo maana
niliposema waende mahakamani, tulitegemea kuna taarifa nyingi
tutaziweka hadharani mahakamani lakini walifuta wenyewe kauli yao
waliyoitoa kwa hiari yao kuwa watanipeleka mahakamani. viashiria hivi
si vya kupuuza hata kidogo katika kulinda mali na rasilimali za Taifa.
Taarifa tulizonazo japo tunaendelea na utafiti unaashiria ufisadi
mkubwa unaendelea bado.
4) Kama nilivyosema, Kodi na ushuru tunaofuatilia sio wa Magari mia
mbili tu, tumepata nyaraka nyingi zinazoashiria, hata Mahindra za 2005
na vifaa vingine vilivyotumika katika kampeni za uchaguzi wa 2005 nazo
hazikuwa zimelipiwa ushuru na Kodi. Ndiyo maana tumepiga kelele kuhusu
mchakato wa ukwepaji uliokuwa unaendelea katika uagizaji wa Magari
200. Ni dhahiri kama tusingelitoka hadharani, wala wasingeliweka
hadharani na wangelipata mwanya kama ilivyo desturi zao( na ninaposema
hivi ni kwa vile nimekwisha kutoa katika michango yangu mingine aina
ya hujuma zilizofanyika mathalan katka uchaguzi wa Serikali za Mitaa,
2009.
You Are Here: Home - - Sakata la Uingizaji magari nchini na kukwepa kodi lajibiwa...
0 comments