Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Polisi watibua ujio wa Drogba, wenzake

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Polisi watibua ujio wa Drogba, wenzake
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwazuia waandishi wa habari na wapiga picha za habari waliokwenda uwanja wa ndege wa kimayaifa wa Julius Nyrere kushuhudia ujio wa timu ya taifa ya Ivory Coast jana

Jessca Nangawe

UJIO wa timu ya taifa ya Ivory Coast, The Elephants nchini umegeuka uhasama baina ya vyombo vya usalama na wanahabari huku mashabiki waliofurika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tangu jioni wakiwa na hamu ya kuwaona nyota hao wakiduwaa.

Mashabiki hao kwa mamia wakiwa na hamu ya kuwaona nyota hao wa wakiongozwa na Didier Drogba, Solomon Kalou na wenzao, walikosa uvumilivu na kuanza kubishana na askari wa kikosi cha FFU waliokuwa wametanda uwanjani hapo na kusababisha vurugu.

Tofauti na ilivyoelezwa awali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambao ni wenyeji kuwa timu hiyo ingewasili saa 12.00 jioni, lakini muda rasmi wa kuwasili uligeuka kuwa jambo la kubashiri na kuwasili hadi saa 1.30 walipowasili.

Kutokana na kusubiri huko, wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliokuwapo pia uwanjani nao walijikuta katika mzozo mkali na askari polisi waliokuwa wakiwazuia wasikaribie chumba cha watu maarufu, VIP katika uwanja huo.

Matokeo yake, ilikuwa vigumu kwa wanahabari kupata nafasi ya kufanya mahojiano na nyota hao ambao walikuwa na hamu ya kuzungumza na kuondoka huku wakiwapungia mashabiki mikono.

Kabla ya wachezaji hao kuondoka, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera aliingilia kati na kuwasihi wanahabari wakutane na nyota hao kwa muda, lakini hilo halikuwezekana kutokana na hasira ambazo zilikuwa zimewapanda huku uongozi wa TFF ukishindwa kusimamia zoezi hilo na kuwaachia FFU.

Nyota hao wa Coast waliondolewa uwanjani hapo kwa basi la timu ya Azam badala ya magari ya TFF, kitendo ambacho kiliamsha manung'uniko kwa mashabiki.

Mwakalebela alijikosha na kuomba radhi akieleza kuwa nyota hao wataongea na wanahabari leo.

Timu hiyo inatarajiwa kesho, Jumatatu kumenyana na Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku mbili baadaye, timu hiyo ya Ivory Coast itachuana na Amavubi ya Rwanda ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Jumanne mahsusi kwa mchezo huo.

Tags:

0 comments

Post a Comment